Thursday 28 May 2015

USIKOSE KUFUATILIA MAZUNGUMZO YANGU KWA WATANZANIA,KUOMBA RIDHAA YA KUWANIA URAIS WA JMT

Ndugu,Watanzania,Napenda kuwajulisha kuwa Tar.31.05.2015 siku ya Jumapili,Nitazungumza na Watanzania kutoka Makao Makuu ya Nchi-Dodoma.
Mazungumzo yangu nanyi yatajikita kuomba ridhaa ndani ya Chama ya Kugombea nafasi ya Urasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tukiwa tunaianza safari ya Kuelekea Miaka 50 tena ya Taifa letu,Naomba usipitwe na Mazungumzo yangu yatakayokuwa LIVE kupitia Redio na Televison Mbalimbali hapa Nchini.
 
Muda: Saa 9 Alasiri hadi 12 Jioni
Mahali:Chuo Cha Mipango Dodoma
Ukumbi:Mwl.Nyerere Hall
 
"WAKATI NI SASA,MABADILIKO KWA VITENDO"
 

No comments:

Post a Comment