Na Mwandishi wetu,Namtumbo Ruvuma.
Kwa ukakamavu kijana wa CCM
akimvisha kitambaa Mh.Mwigulu nchemba mara baada ya kuwasili kwenye
kambi ya mafunzo ya vijana wa CCM-Namtumbo
CCM oyeeeeee!!!Naibu katibu mkuu akisalimiana na vijana wa CCM wakati akiingia eneo la tukio.
Naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara
ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi Mh.Mwigulu Lameck Nchemba leo
Tar.31/10/2013 amefunga rasmi mafunzo ya vijana wa CCM (UVCCM)
yaliyofanyika kwa muda wa wiki mbili hapa Ruvuma Wilaya ya
Namtumbo.Mafunzo haya yaliyojumuisha wilaya zote za Ruvuma kwa vijana wa
CCM yalilenga kuwajengea uwezo vijana wa kutambua Umuhimu wao katika
kushiriki kwenye shughuli za maendeleo ndani ya nchi yao,siasa za nchi
na mwenendo wake,Uelewa kuhusu namna ya kufanya maamuzi sahihi katika
umri wake huu wa ujana,pia kuwaandaa kifikra na kimaadili kwaajili ya
kuijenga na kuimarisha CCM pamoja na jumuia zake hasa Umoja wa Vijana wa
Chama cha Mapinduzi.
Vijana wakiwa na nyuso za Furaha baada ya kuonana uso kwa uso na Kiongozi wao wa chama wa ngazi ya taifa.Mh.Mwigulu nchemba
Akizungumza kwa mifano mingi iliyohai
ndani na nje ya nchi yetu,Mh.Mwigulu Nchemba wakati wa kufunga mafunzo
ya vijana wa CCM amezungumza na vijana wote waliokuwepo kambini(Vijana
450) na kuwasihi sana kuwa makini na mambo makuu matatu,Moja ni
kuhusiana na Uandishi wa katiba mpya,Pili amezungumzia kuhusu rasilimali
za nchi na mwisho amesisitiza kuhusu Umuhimu wa vijana kujitambua hasa
ukizingatia Taifa letu linapita katika kipindi aambacho vijana ni wengi
sana kuliko rika lolote lile.
Hapo vipiiii???ni ishara ya dole(mambo sawa) kutoka kwa Naibu katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi.
Akianza kwa kuzungumzia Mchakato wa
uandishi wa katiba Mpya,Mwigulu Nchemba amewaomba vijana kuwa makini
sana na propaganda zozote zile wanazozisikia kutoka kwa watu wengine
kuhusu kufanya vurugu ili katiba isipatikane.Amesema mchakato wa katiba
umekwenda vizuri na umezingatika matakwa ya kila kundi na Taasisi licha
ya Taasisi zingine kutaka maoni yao yawe bora kuliko ya watu
wengine,"Katiba hii si ya CCM na sio ya chama chochote kile au mtu
yeyote yule ni katiba ya Watanzania wote bila kuangalia
rangi,kabila,chama,maumbile ya mtu n.k .Maoni yamekusanywa na kufanyiwa
tathimini na tume husika na sasa tunaelekea hatua za mwisho za kupata
katiba mpya.Hivyo basi nawaomba sana vijana wa CCM na vijana wengine
wote kuacha kujiingiza kwenye makundi na mkumbo wa kugomea mchakato wa
katiba mpya,kwa sababu hao wanaowahimiza kugoma wao wenyewe wanaajenda
yao ya siri kuhusu Taifa hili.Ni kawaida yao kugoma,ni kawaida yao
kupinga kila kitu,Kila mmpja wetu alipewa nafasi ya kutoa maoni kupitia
taasisi na wanachama wake,Kuna wenzetu walikuwa wanafanya mikutano ya
hadhara,hii yote ni kuhadaa na kudanganya watanzania."alisema.
Namshukuru sana Rais kikwete kwa kuwapa
somo wapinzani kwamba maandamano si suruhisho na jambo lolote zaidi ya
kudumaza maendeleo,Yawezekana walikuwa natafuta sehemu ya kula ruzuku za
vyama vyao sijui!!Lakini tujiulize ni mapenzi gani haya ya jioni?Ni
ndoa gani hii ya watu watatu ya usiku?Wapi na wapi hawa watu wakaungana
eti kutetea maslahi ya Watanzania.?.
Hivyo nawaomba sana vijana muache kabisa
kabisa kujihususisha na uvunjifu wa amani au kugomea jambo lolote la
kitaifa.Kama linakwenda vibaya vyombo vya kusemea vipo na serikali
inawapa nafasi hiyo.
Jambo kuwa nawahakikishieni vijana wa
CCM,Kwa namna CCM tulivyoimara iwe kwa katiba ya sasa au mpya au katiba
yoyote CCM tutashinda kwa sababu tunajiamini,tunakubalika kwa
watanzania,tunamtandao mkubwa sana na jumuia yetu moja tu kama hii ya
vijana ni kubwa kuliko CHADEMA yote na vyama vingine.
Vijana wakifurahia jambo kutoka kwa mgeni rasmi Mh.Mwigulu Nchemba
Jambo la pili Mh.mwigulu Nchemba
amezungumzia kuhusu rasilimali za nchi na namna vijana wanatakiwa
watumie fursa husika kuzilinda mali na kujitengenezea mazingira ya ajira
kwa siku za karibuni.Mwigulu amewasisitizia vijana kuwa serikali
imejenga barabara kutoka Dsm hadi Namtumbo kwa kiwango cha rami na
barabara hiyo imeunganishwa mikoa yote ya Tanzania.Hivyo rasilimali za
nchi ni lazima zilindwe ilikunufaisha wazawa/watanzania wote na sio watu
wachache.Ameomba vijana kulinda rasilimali za nchi yao na kauchana na
wajasiliamali wa mataifa makubwa ambao wamekosa uzalendo ndani ya nchi
yetu na wanaingia mikataba ya vyama vya nje ya kuwapa masharti eti
wakichukua dola watagawana rasilimali zilizopo.
Naibu katibu mkuu akitoa kadi ya uanachama wa UVCCM kwa mmoja wa vijana wa CCM waliohudhuria mafunzo hapa Namtumbo.
Swala la ulinzi na usalam wa Taifa letu
ni la kila mmoja wetu vijana,hakuna kuwapa nafasis watu wasio litakia
mema taifa letu.Serikali ya CCM imejipanga kuhakikisha rasilimali
zilizopo zinanufaisha wananchi wote.zinalindwa kwa namna yoyote
ile.Nimesikia kuwa kuna wasiasa wanakuja kuwaomba mfanye maandamano na
vurugu kuhusu mali za nchi yenu,Wapuuzieni hao kwasababu nyie wenyewe
mnaona kazi zinazofanyika na serikali yenu na namna rasilimali
zinavyotumika kwa manufaa yoyote.Hapa Namtumbo na mkoa mzima wa Ruvuma
miradi ya serikali ya mingi imeshatekelezwa ya barabara,Umeme na afya
ambayo ni kazi ya serikali ya CCM kupitia kodi na manufaa ya rasilimali
zetu.Naomba sana mtumie ujana wenu kulinda mali za nchi na kuipigania
CCM iendelee kuongoza nchi yetu kwa miaka mingi zaidi kwa sababu nje ya
CCM vyama vingine ni wababishaji tu na wanajenda zao na ndugu zao huko
kwenye mataifa ya nje.
Mh.Mwigulu Nchemba akizungumziza na mamia ya vijana wa CCM wakati wa kufunga mafunzo.
Msiwe kama watu wa Misri ambao hadi leo
hawalewi wanachokihitaji,kwa sababu walimuondoa Rais wao wa aliyekuwepo
madarakani,wakamuweka wakwao,ndani ya miezi sita wamemng'oa waliomuweka
wanasema bora yule wa kwanza.Leo hii ukiwauliza wanataka nini
watakwambia hata hawajui wanataka nini.Nchi yao imeshagawanyika na amani
hairudi tena kirahisi.
Tatu,Naibu katibu Mkuu ametoa somo kwa
vijana wa CCM namna ya kuendana na hali halisi ya Taifa letu hasa idadi
kubwa ya vijana kuliko rika lolote ndani ya nchi.Vijana ni wengi sana na
wengi hawana ajira za kutosheleza mahitaji yao.Hivyo wingi wa
vijana,Mh.Mwigulu anasema ni lazima vijana watumia muda na akili zao
vizuri ilikuepukana na makundi hatarishi ya tabia na maisha
yao,kujiepusha na vyama vinavyohangaika huku na kule kuhakikisha nchi
yetu haitawaliki.
Zaidi ya vijana wa CCM 450
waliokaa kambi wiki mbili kujifunza namna ya kuongoza,siasa na utendaji
wakimsikiliza Mh.Mwigulu Nchemba.
Nanukuu"Nimekuwa kijana kama
nyie,nimepitia umoja wa vijana wa chama changu cha CCM,Nilijituma
kujihusisha na kazi za maendeleo ya chama na nchi yangu,Niliepukana na
makundi yasio na tija kwangu na nilitii kile wakubwa walichonielekeza
ndio maana leo nimefikia katika hatua kubwa kama hii ya uongozi nikiwa
bado kijana"Hivyo basi nanyie mnayonafasi ya kuhakikisha mnakuwa watu
wema katika jamii yetu,mfano wa kuigwa,na hasa nategemea mafunzo haya
yamewapa somo kubwa sana na mmeelimika vya kutosha namna ya kuwakiongozi
na mtendaji mzuri kuanzia ngazi ya familia,Shina,tawi n.k kwa CCM.
Mh.Mwigulu Nchemba akimtunuku
mmoja wa vijana wa CCM, kuthibitisha kuwa amehudhuria mafunzo ya
utendaji na uongozi wa umoja wa vijana.
Umoja wa vijana ndio siraha ya
chama,mnategemwa sana kuzalisha viongozi wajao kutoka kwenye kundi
hili.Nimeshawaona warithi wa Komba hapa(uimbaji),warithi wa Jenista
Mhagama(uongozi) akina Dr,Emmanuel Nchimbi wapo hapa na hata Mh.Vita
kawawa wingine yupo hapa.
Hivyo basi mnakila sababu ya kuendelea
kuitetea CCM na kuhakikisha mnalinda heshima yake kwa nchi na nje ya
nchi.hatupendi CCM kuwa kama vyama vingine ambavyo wezi
wastaafu,wazinzi,mwenyekiti wake anapigana ngumi na mwenyekiti mwenzake
hao wote kwao wanajiita makamanda na majembe.
Mh.Mwigulu nchemba akisalimiana na kuzungumza machache na moja ya Mzee wa CCM anayeishi wilaya ya Namtumbo-Ruvuma.
CCM tunahitaji kuona makamanda wakweli na majembe ya kweli kama akina Nape Moses Nnauye,Sixtus mapunda na vijana wote wa UVCCM na viongozi wake wakizaliwa kutoka miongoni mwenu vijana wa Ruvuma.
Ni rai yangu kwako kijana wa CCM na
wakitanzania kuwa baada ya mafunzo haya kila mmoja wenu atakwenda kuwa
mwalimu kwa mwenzake huko muendako.CCM ipo pamoja nanyi na hatuwezi
kuipoteza benki hii ya vijana na tunaanza miradi mbalimbali ya chama
kupitia kwenu.
Mbunge wa Namtumbo Vita kawawa akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Mwigulu nchemba
Naye,Mbunge wa Namtumbo Mh.Vita Kawawa
aliyekuwa mwenyeji wa Mh.Naibu katibu mkuu alizungumza na vijana
waliomaliza mafunzo yao kwa kuwambia "Wote mliopo hapa mmeona maendeleo
yanayofanyika huku Ruvuma na hasa hapa Namtumbo,Mwaka 2010 hatukuwa na
rami wala umeme,Leo tuna rami na umeme hapa.Naomba uchaguzi ujao muwe
vinara wa kuifanya CCM iendelee kuongoza jimbo hili na dola ya nchi
yetu.Vijana wenzangu huu ni muda wa kupambana sana na wapinzani
wetu,hawana sera zaidi ya kusuka mipango ya kuharibu amani ya nchi na
kufanya nchi isitawalike.Ilani ya CCM imetekelezwa ipasavyo na mnahaki
ya kusimama na kuitetea CCM popote pale.Nipo tayari kuwasaidia kufanya
mipango endelevu ya kujenga chama pamoja nanyi vijana wenzangu".
Mbali na kuwa mgeni rasmi kwenye kufunga
mafunzo ya vijana wa CCM hapa Namtumbo,Naibu katibu mkuu alipata nafasi
ya kutembelea ujenzi wa ofisi za chama cha mapinduzi wilaya ya
Namtumbo,ofisi kubwa wenye kujuisha jumuia zote za chama,car wash,Ukumbi
wa mikutano na maeneo ya biashara(miradi ya chama).
Mh.Mwigulu Nchemba akiingia
kwenye ofisi za CCM wilaya ya Namtumbo,ofisi mpya ambazo bado
zinaendelea kujengwa.Kushoto ni katibu wa CCM wilaya ya Namtumbo.
Mwigulu alitumia fursa hiyo kuwapongeza
sana viongozi wa chama kuanzia ngazi ya mkoa,wilaya na had ngazi ya
chini kabisa kwa namna wanavyoendelea kuijenga CCM na kuiimarisha ndani
ya mkoa wa Ruvuma.
Wilaya ya Namtumbo ni mpya ikiwa na
miaka saba(7) sasa tangu ianzishwe na Mbunge wake ni Vita Kawawa ambaye
alikuwa mwenyeji wa Mh.Mwigulu Nchemba siku ya leo.CCM inashikilia kata
zote za wilaya ya Namtumbo na inashikiliza vijiji vyote (serikali za
mitaa).Hivyo CCM ndicho chama pekee kinachoongoza wilaya nzima ya
Namtumbo.
Naibu katibu mkuu akipewa
maelekezo kutoka kwa katibu wilaya ya Namtubo wa CCM kuhusu maendeleo ya
ujenzi wa ofisi za kisasa za chama.
Mapenzi kwa chama kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto.Mh.Mwigulu alimzawadia hicho alichokishika mtoto mkononi.
Pia alipata wasaha wa kukutana na Mkuu
wa mkoa wa Ruvuma Mh.Said Thabit Mwambungu ambapo walizungumzia hali ya
maendeleo ya wilaya na hali ya kisiasa ndani ya mkoa wa Ruvuma.
Naibu katibu Mkuu alipomtembelea
Dc wa wilaya ya Namtumbo ofisini kwake kabla ya kuelekea kwenye ufungaji
wa mafunzo ya vijana wa CCM.
No comments:
Post a Comment