Sunday 13 April 2014

TASWIRA,MH:MWIGULU NCHEMBA ALIPOTEMBELEA SHUGHULI ZA MAENDELEO NA KUTOA MREJESHO WA AHADI ZAKE KATA YA NTWIKE

Mh:Mwigulu Nchemba akisaidia Kupandisha Udongo kwa Mafundi wakati alipotembelea Kukagua Ujenzi wa Maabara ya Kisasa Shule ya Sekondari Ntwike hii leo Jimboni Kwake Iramba.Jengo Jipya la Maabara ya Kisasa kwa Sekondari ya Ntwike.Mh:Mwigulu Nchemba akicheza Ngoma ya asili na Wananchi wa Kijiji cha Mingela wakati amewasili kwaajili ya Mkutano wa Hadhara wa Maendeleo.Mh:Lusinde(Mbunge wa Mtera) akibadilishana Mawazo na Mh:Mwigulu Nchemba kwenye Mkutano wa hadhara kijiji cha Mingela.
Mh:Mwigulu Nchemba akisikiliza neno Kutoka kwa Mwananchi wa Kijiji cha Mingela kata ya Ntwike.
Mh:Mwigulu NChemba Mbunge wa Iramba akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Mingela hii leo Alipokwenda kutoa mrejesho wa ahadi yake ya Maji na Umeme,Maji yameshaanza Kupatikana Kupitia Mradi Mkubwa wa Kisima kilichochimbwa kwa Mfumo wa Kisasa ndani ya Kijiji hicho,Pia Kijiji hicho kipo kwenye Mpango wa Kupatiwa Umeme kabla ya Mwezi wa sita Mwaka 2015.Mh:Mwigulu Nchemba akiwaonesha Gari Wananchi wa Kijiji cha Nkongilangi aliyowanunulia kwaajili ya Huduma za Afya kwenye Tarafa yao ya Shelui.Gari hiyo ya Wagonjwa itatumika Bure kwa Wananchi bila Kuchangishwa Mafuta.
Sehemu ya Mamia ya Wananchi wa Kijiji cha Nkogilangi waliofika kwenye Mkutano wa Hadhara wa Kupokea habari njema za Maendeleo ndani ya Kata yao kutoka kwa Mh:Mwigulu Nchemba Mbunge wao.
Wananchi wa Kijiji cha Nsusu ambao wanategemea Kupata Umeme wakishangilia baada ya Kusikia Juhudu hizo za Mbunge wao Mh:Mwigulu Nchemba.
Mh:Diwani wa Kata ya Ntwike akitoa Mrejesho wa Maendeleo kwa Wananchi mbele ya Mbunge wa Iramba Mh:Mwigulu Nchemba,Kubwa ni Ujenzi wa Barabara ya Kutoka Nsusu kuelekea Kiomboi kukatisha Mlimani,Pia Ujenzi wa Maabara ya Kisasa kwa Sekondari ya Ntwike.Pia Diwani ametoa Ushuhuda namna Kata yake inavyonufaika na Mfuko wa Jimbo,Mh:Mwigulu Nchemba ametoa fedha mara kadhaa kusaidia Maafa ya Kuezuliwa Shule na Makazi ya Watu ndani ya Kata ya Ntwike.Hapo awali Wananchi na Viongozi walikuwa hawajui Mfuko wa Jimbo na Matumizi yake,Wamejua hilo baada ya Mh:Mwigulu Nchemba kuwa Mbunge.Kada Mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi Kutoka Kitengo cha Uhamasishaji wa UVCCM Bi.Juliana Shonza akiwasalimia Wananchi wa Kijiji cha Nsusu.
 Wananchi wanapofurahia Kukutana na Mbunge wao baada ya Kupokea habari Njema za Maendeleo ndani ya Kata yao,Maji,Umeme,Afya na Barabara vyote vimeshaanza kutekelezwa kwa Vitendo na Wananchi wanashuhudia Utekelezaji huo.Wananchi wakitafuta Kila Namna kuhakikisha Wanamuona Mbunge wao,Hapa ni Kijiji cha Nkogilangi kata ya Ntwike.
Kwa herini Wananchi Wangu"Msitamani sana Kuniona mimi kwenye Kata yenu,Tamaa Yenu ielekezeni kuona Shughuli za Maendeleo zinaonekana na Kufanyika kwa Ufanisi ndani ya Jimbo letu"Mwigulu Nchemba.
 Picha/Maelezo na Sanga Festo

No comments:

Post a Comment