Hii
ndio Gari ya Wagonjwa(Ambulance) aliyonunuliwa na Mh:Mwigulu Nchemba na
Kuwakabidhi Wananchi wa Tarafa ya Shelui kwenye Kituo Kikubwa cha Afya
cha Mgongo.Naibu Waziri wa Afya Mh:Kebwe akijianda Kupanda kwenye Gari la Wagonjwa tayari kwa Kulizindua rasmi kwakaunza kutumika na Wananchi wa Tarafa ya shelui,Gari limenunuliwa na Mh Mwigulu Nchemba kwaajili ya Kituo cha Afya cha Mgongo.Naibu
Waziri wa Afya Mh:Kebwe Stephen Kebwe akionesha Ufungo wa Gari ya
Wagonjwa na Kuukabidhi kwa Wananchi kupitia Mkurugenzi wao wa Wilaya.Mh:Mwigulu Nchemba Mbunge wa Iramba akikabidhi kadi halali ya Umiliki wa Gari ya Wagonjwa kwenda kwa Wananchi.Naibu
Waziri wa Afya Dkt Kebwe Stephen Kebwe akimkabidhi Ufunguo wa Gari
Mkurugenzi wa Wilaya ya Iramba tayari kwa kuanza Kusimamia Matumizi ya
Gari hilo mali ya Wananchi.Naibu Waziri wa Afya akisalimiana na Wananchi wa Kyengege waliojitokeza Kumpokea,Ameambatana pia na Mkuu wa Wilaya ya Iramba na Mbunge wa Iramba Mh:Mwigulu NchembaNaibu
Waziri wa Afya Mh:Kebwe Stephen Kebwe akizindua rasmi Nyumba ya
Watumishi wa Kituo cha Afya Kata ya Kyengege Jimbo la Iramba,Pia Kutoka
Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mh:Yahya Nawanda na Mbunge wa Jimbo
hilo Mh:Mwigulu NChemba.Hii ndio Nyumba ya Watumishi wa Kituo cha Afya cha Kyengege iliyozinduliwa na Naibu Waziri wa Afya.Kituo Cha Afya cha KyengegeNaibu
Waziri wa Afya(Katikati) akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Iramba
Mh:Yahya Nawanda na Mbunge wa Jimbo hilo Mh:Mwigulu Nchemba wakielekea
kukagua maendeleo ya Kituo cha Afya cha Kyengege hususani kwenye kitengo
cha Dawa.Wananchi
wa Kata ya Kyengege wakifurahia Kupata Nyumba ya Watumishi wa Kituo cha
Afya,Awali Wananchi hawa walipangisha Nyumba kwaajili ya Kuishi
Watumishi hao.Mh:Lusinde Mbunge wa Mtera akizungumza na Wananchi wa kata ya Kyengege kuhusiana
na Umuhimu wao Kushiriki kwenye kazi za Maendeleo hususani mambo ya
Afya,Pia Kuwashuhudia namna Mh:Mwigulu Nchemba anavyolitumikia Taifa
lake, Chama chake na hadi Jimboni Kwake.Amewasihi kutothubutu kuacha Kumuunga Mkono Mwigulu Nchemba,Wananchi Waendelee kumuunga mkono kipindi chote cha Uongozi wake."Msipende sana Kuiniona Mimi Mbunge wenu,Pendeni sana Kuona Maendeleo yanakuja na yanaonekana"Mmoja ya Watumishi wa Kituo cha Afya cha Kyengege(Jina hakufahamika) akifurahia Kupata Nyumba nzuri ya Kuishi.Mh:Mwigulu
Nchemba akizungumza na Wananchi wa Shelui kuhusu namna alivyotekeleza
ahadi yake ya Kuwapatia Ambulance itakayosaidia Kuwahisha Wagonjwa
kupata Matibabu kwenye Hospitali Kubwa za Igunga au Kiomboi-Iramba.
Wananchi
wa Kijiji cha Mgongo wakishangilia kwa Furaha mara baada ya Kukabidhiwa
Gari ya Wagonjwa kutoka kwa Mbunge wao Mh:Mwigulu Nchemba.Katika Kata
hii ya Mgongo,Mh:Mwigulu Nchemba wakati anaomba ridhaa ya Kuwaongoza
Wananchi hawa aliwaahidi kuwapelekea Umeme,maji na Gari ya Wagonjwa,hadi
sasa Mbunge huto ametekeleza Vyote alivyoahidi na amewaahidi kuanza
kuwashughulikia uboreshaji wa Barabara.
Mamia
ya Wananchi wa Shelui wakiwa wamejitokeza kwa wingi kushuhudia tendo la
Kukabidhiwa Gari waliyopewa na Mbunge wao Naibu Waziri wa Fedha
Mh:Mwigulu Nchemba.Naibu Waziri wa Afya Mh:Kebwe akimuchunguza Mama mwenye tatizo la tezi Shingoni na Kumuagiza Daktari wa Wilaya ya Iramba kuhakikisha anapekelekwa Hospitali kwa Matibabu zaidi.
Mh:Mwigulu
Nchemba akiwa na Mwananchi wa Kijiji cha Mtoa mwenye tatizo la tezi
Kuvimba,Hapa akitoa fedha kwaajili ya Nauli ya Mama huyo kwaajili ya
Kufuata Matibabu sehemu atakayopelekwa na Daktari wa Wilaya aliyeagizwa
na Naibu Waziri wa Afya ahakikishe mama huyo anapata Matibabu Stahiki.Wananchi wa Kata ya Mgongo wakimpokea kwa Shangwe Mbunge wao Mh:Mwigulu Nchemba.
Katika
hali inayoonekana ni Wazi kuwa Mh:Mwigulu Nchemba amejikita Kutimiza
ahadi zake alizotoa kwa Wananchi wa Jimbo la Iramba,Hii leo amekabidhi
Gari mpya ya Wagonjwa kwenye Tarafa ya Shelui Kituo cha Afya cha
Mgongo.Hii ilikuwa ni moja ya ahadi zake wakati anaomba ridhaa ya
Kuwaongoza Wananchi wake,Ameshawapelekea Umeme,Maji na sasa
alimewakabidhi Gari ya Kubebea Wagonjwa katika Kituo hicho cha Afya.
Ikiwa
ni Wiki moja tu tangu Mbunge huyo afanye Ziara na Mh:Waziri wa Nishati
na Madini Mh:Mhongo kukagua Utekelezaji wa Mradi wa Umeme katika Vijiji
43 ndani ya Jimbo la Iramba Unaotegemewa Kukamilika Mwezi wa Sita
2015,Na Baadae Mbunge huyo ndani ya Wiki hiyo hiyo Moja alifanya ziara
na Waziri wa Maji Mh:Maghembe na Kufungua baadhi ya Miradi ya Jimboni
hapo Ukiwamo ule Mradi Mkubwa wa Maji Uliokamilika wa Nang'uli
Mh:Mwigulu
Nchemba ameendelea Kusisitiza kuwa Mkataba wake na Wananchi wa Jimbo la
Iramba ni Shughuli za Maendeleo,alipewa ridhaa ya Kuwaongoza
iliawaletee Maendeleo kwa Vitendo,Hilo amekuwa akilifanya Jimbo la
Iramba kwenye Seketa zote hususani Elimu,Afya,Umeme,Maji na Barabara.Kwa
sehemu Kubwa ametekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi ndani ya Jimbo
lake na sasa anajipanga Kujikita kwenye Kuboresha Barabara ya Kutoka
Ndago Kupita Mbelekesye Kuja Singida,Kuboresha barabara ya Kidalu
kuelekea Meatu n.k.
Kwa
Nyakati tofauti Wananchi kwenye Mikutano ya hadhara wamekuwa
wakishindwa kujizuia kutoa shukrani zao za dhati kwa Mh:Mwigulu Nchemba
kwa namna alivyowasaidia kwa muda mfupi tu kwenye shughuli za Maendeleo
na Kwenye Kutatua Matatizo ya Watu binafsi na Jumuia.
Habari/Maelezo na Sanga Festo
Mh Mwigulu binafsi nakuunga mkono maendeleo ya mwanachi yanapatikana pale ambapo afya inakuwa imara na tiba inapopatikana kwa wakati. Pia nakushauri wekeza sana kwenye kuwachangia vijana walio jiajiri kwenye vikundi kama Wa endesha bodaboda wawe na duka lao la umoja la spare za pikipiki, Saccoc za wakina mama wanapohitaji msaada, Saccoc za wafugaji na wakulima wawezeshe kupata misaada ya madawa ya mifugo na kilimo, washirikishe wamiliki wa viwanda vya mbolea na dawa za mifugo kukupa vyanzo vya misaada.Binafsi ndio nimeanzisha UMOJA wa mafundi umeme Kigoma wapo zaidinya 145, Umoja wa mafundi Ujenzi zaidi ya 220 na sasa nakamilisha andiko la Umoja wa waendesha Bodaboda zaidi ya 2700.Namshukuru sana Mchumi wa Mkoa ananipa ushirikiano mkubwa.Mwakani najiandaa kuchukua fomu ya Ubunge
ReplyDelete