Wednesday, 10 August 2016

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI,ATEMBELEA KAMBI TATU ZA WAKIMBIZI MKOANI KIGOMA


Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi,Mh:Mwigulu Nchemba akiwa na Mkuu wa wilaya wa Buhigwe(Kushoto) Col.Martin Gaguti na Mkuu wa wilaya wa Kasulu Col.Mkisi alipowasili mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.Kikao cha askari wa magereza,zimamoto,polisi na uhamiaji kikiendelea wakati Mh:Mwigulu nchemba alipokutana nao kwaajili ya kuwaleza dira ya wizara yao na changamto ilizopanga kuzitatua.Mwigulu Nchemba akipewa maelezo kuhusu idadi ya wakimbizi waliopokelewa tangu kuanza kwa mwaka huu wakitokea Burundi.Ambapo kwa takwimu za awali kuna wakimbizi zaidi ya laki moja mkoani kigoma waliowekwa kwenye makambi matatu tofauti.Waziri wa mambo ya ndani akisalimiana na mmoja ya wakimbizi waliopo kwenye kituo kidogo cha Kigoma mjini wakisubiri safari ya kuelekea nchini Marekani na Sweeden kwaajili ya hifadhi.Mwigulu Nchemba akifurahia jambo na wakimbizi wanaoandaliwa kwaajili ya safari ya nje ya nchi kwaajili ya hifadhi.Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Col.Martin Gaguti akimpatia maelezo mbalimbali Waziri wa mambo ya ndani alipowasili kwenye mpaka wa manyovu unaotenganisha Tanzania na Burundi.Changamoto ya wakimbizi kutoroka na kurudi nchini kwao kinyemelea,inawafikisha mikononi mwa Mh:Mwigulu Nchemba ambaye ameshuhudia wakimbizi kadhaa katika mpaka wa Manyovu wakijaribu kurejea Burundi kinyemela bila kufuata taratibu.Mwigulu Nchemba alipowasili wilaya ya Kasulu na kupokelewa na Mkuu wa wilaya Col.Mkisi
Katika hatua nyingine,Mwigulu nchemba alilazimika kukutana na madiwani waliopo wilaya ya kasulu kwaajili ya kuwapa somo na angalizo namna ya kusaidia serikali kukamata wahalifu na wakimbizi haramu wanaotishia usalama wa mkoa wa Kigoma.Hawa ni wakimbizi kutoka nchi jirani ya Congo,hapa wapotayari kwaajili ya kusafirishwa kupelekwa Kigoma kwaajili ya usaili wa kusafirishwa kwenda nchi za Ulaya.Mwigulu Nchemba akiagana na wakimbizi wa Congo kwenye kambi ya Nyarugusu.Akiwa katika kambi ya Nyarugusu,Mh:Mwigulu Nchemba akatembelea wodi ya wazazi kwaajili ya kukagua huduma za afya.Hapa waziri Nchemba amempakata mmoja wa watoto wa wakambizi aliyezaliwa katika Hospitali hiyo iliyopo ndani ya kambi.Mwigulu Nchemba akimsalimia mmoja ya watoto waliozaliwa kwenye kambi ya Nyarugusu.Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na watoto ambao ni wakimbizi waliopo katika kambi ya Nyarugusu -Mkoani Kigoma.Mwigulu Nchemba akisaidia ufyatuaji wa tofali za ujenzi wa makazi ya wakimbizi waliomba hifadhi kwenye kambi ya Nduta wilaya ya Kibondo.Moja ya nyumba za kuhifadhi wakimbizi kwa muda zinazoendelea kujengwa kwenye kambi ya Nduta .Msimamizi(Kushoto )wa shughuli za Shirika la wakimbizi Duniani akitoa maelezo kwa Waziri wa mambo ya ndani namna wanavyojitahidi kuhakikisha mazingira ya wakimbizi katika kambi zote tatu wanapata huduma zote muhimu.Waziri wa mambo ya ndani akizungumza na kamati ya Usalama ya wilaya ya Kakonko alipotembelea kambi ya wakimbizi ya Mtendeli.
Picha/Maelezo na Festo Sanga Jr.

No comments:

Post a Comment