Sunday, 3 November 2013

PICHA,MKUTANO MKUBWA WA MH:MWIGULU NCHEMBA SHELUI--IRAMBA,AMWAGA DAWATI NA AMBULANCE KITUO CHA AFYA SHELUI

Na Mwandishi Wetu.
Naibu katibu CCM Tanzania Bara na Mbunge wa Iramba Mgharibi Mh.Mwigulu Nchemba leo jumapili 3/11/2013 amefanya mkutano mkubwa wa hadhara hapa Iramba kata ya Shelui akizungumza na wananchi wake kuhusu shughuli mbalimbali za maendeleo na kukabidhi madawati kwaajili ya shule pamoja na kutoa taarifa ya kununua Ambulance kwaajili ya wanaShelui ya matumizi ya kubebea wagonjwa kituo cha afya cha Shelui.
Mbunge huyo ambaye kwa muda mrefu sasa ameteka media za nchi kutokana na umahili wake wa kisiasa,akiwa amembatana na Mbunge wa Tabora Mjini amezungumza mambo mengi sana na wanashelui ikiwa pamoja na kuwapa nafasi ya kuhoji na kuuliza maswali mbalimbali ya mwendeo wa siasa na utekelezaji wa Ilani ya CCM.Mwigulu Nchemba amewapongeza sana wakazi na wananchi wa Shelui kwa namna walivyoshiriki kwenye ujenzi wa kituo cha afya ambacho yeye(mwigulu) amechangia mifuko ya cement na mabati.Pia kwa sasa amewanunulia gari la Ambulance kwaajilya wagonjwa,Gari lipo mbioni kuletwa Shelui mapema ndani ya Mwaka huu.

Katika hatua nyingine Mbunge huyo amewaomba Wanashelui kupuuzia kelele zozote za wapinzai za kuhusu yeye,amedai kuwa wapinzani(CHADEMA) wameelekeza nguvu zao kupambana na yeye kwasababu ni tishio kwao na amekuwa mstari wa mbele kufichua maovu wanayofanya na kupanga kuyafanya.Hivyo yeye yupo imara sana na anategemea wananchi wa Shelui hawatatoa nafasi kwa watu waaina hiyo ya CHADEMA.Mwigulu amekwenda mbali zaidi kwa kusema kuwapa nafasi wapinzani nikukaribisha vurugu,uvunjifu wa Amani katika kata yao,Wapinzani ndani ya vyama vyao wanapigana ngumi mwenyekiti kwa mwneyekiti na mmeona namna walivyosababisha kifo cha kijana pale Ndago,walivyomwagia tindikali kijana(Musa Tesha)pale Igunga n.k.alisema Mwigulu.
Vijana endeleeni kujishughulisha na kazi za maendeleo,endeleeni kujikusanya kwaajili ya kutoa misaada ya bodaboda na mikopo kama nilivyofanya kwenye kata zingine,Naomba mshiriki kwenye michezo hasa hii michuano yangu niliyoanzisha.Kukaa bila kazi ni hatari sana kwa kijana ndio maana mnakuja kujiingiza kwenye vyama visivyo na mwelekeo wowote hapa nchini"Mwigulu.
Jambo kubwa la kufurahisha katika Mkutano huu Mh.Mwigulu Nchemba alitoa nafasi kwa wananchi kutoa dukuduku zao,mawazo na maswali ya mambo mbalimbali yanayowakabili.Maswali yote yalijibiwa na mengine kujibiwa na watendaji moja kwa moja,Hatua hii imetoa fursa kwa wananchi kujua mambo mengi hasa matumizi ya mfuko wa jimbo ambapo wengi wao walikuwa hawajui kuwa Mbunge hakutani na fedha ya Mfuko wa jimbo zaidi ya Ofisi ya waziri mkuu na mkurugenzi wa wilaya na kisha kwenda kwa mfumo wa cheki kwenye serikali za vijiji.
Mengi zaidi tazama kwenye picha hapa chini.

 Mwigulu Nchemba akishiriki kucheza ngoma ya asili ya kinyiramba na mmoja ya mwimbaji wa kundi la ngoma za asili hapa Shelui

 Mh.Mwigulu Nchemba akisalimiana na wananchi wake wa kata ya shelui hii leo kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara uwanja wa Shelui stendi.
 Mbunge wa Iramba Maghariobi akiwatuliza wananchi wasiendelee kushangilia mafanikio yake aliyokuwa akiwaeleza hususani utekekelezaji wa Ilani ya CCM.Mwigulu Nchemba ametolea ufafanuzi wa Ujenzi wa Kituo cha kisasa cha afya kata ya Shelui wakati huo huo Mbunge huyo ametoa Gari la AMBULANCE kwaajili ya matumizi ya wananchi wa kata ya Shelui.
Kabla ya kutoa taarifa ya kuwapatia gari ya Ambulance kwaajili ya wagonjwa,Mbunge huyo amechangia mifuko 30 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya na huku akitoa mabati zaidi ya miatano kwaajili ya ujenzi wa nyumba za Ibada na Vituo vya afya wilaya ya Iramba.
 Mh.Aden Rage akishuka jukwaani mara baada ya kuongea na wananchi wa Shelui kuhusu namna ya kutunza rasilimali watu walizonazo.Rage amewaomba wananchi wa shelui kuhakikisha hawafikirii hata kumchagua mgombea yeyote nje ya Mwigulu nchemba kwasababu ni Mbunge kijana mchapa kazi na mwenye uwezo mkubwa wa kutatua matatizo ya wananchi wa Iramba na watanzania kwa ujumla,Pia Mbunge huyo wa Tabora mjini na Mwenyekiti wa Simba Sport Club ameweka bayana kuwa Ilani ya CCM imetekelezwa kwa kiwango kikubwa sana hivyo haoni sababu ya Watanzania kufikiria kubadilisha serikali au wabunge wa CCM waliopo madarakani.
 Mh.Mwigulu nchemba akiwa na Mh.Aden Rage pamoja na diwani wa Shelui na mwenyekiti wa wanawake kata ya Shelui.
 Kazi ilikuwa kubwa sana kumuondoa Mh.Mwigulu Nchemba eneo la Mkutano kutokana na umati mkubwa wa wananchi kutaka kumbeba na kusukuma gari lake hadi eneo la barabara iendayo Igunga.
 Mara baada ya kumalizika kwa mkutano,Mh.Mwigulu Nchemba alipokelewa kwa mbio na vigelegele toka kwa wananchi wake wa Shelui kumpongeza kwa namna anavyowasaidia kutatua kero na shida mbalimbali zinazowakabili katika shughuli zao za maendeleo.
 CCM OYEEEEE!!!!
 Msaada wa kumuondoa eneo la mkutano linaendelea hapa kwa kusaidiana na viongozi wengine wa CHAMA na serikali za mtaa hapa shelui ili awezekuwahi ratiba zingine za kazi za maendeleo ndani ya jimbo lake la Iramba Magharibi.
 Hii ni sehemu ya Mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye Mkutano wa hadhara wa Mh.Mwigulu Nchemba kata ya shelui ndani ya jimbo lake la Iramba magharibi.

 Katika hatua nyingine Mbunge wa Iramba Mh.Mwigulu Nchemba amekabidhi dawati 20 kwaajili ya shule ya msingi moja wapo hapa Shelui.Kwa dawati hizi 20 Mbunge huyo atakuwa amefikisha dawati 60 ambazo wananchi waliomba kwaajili ya kutatua swala la watoto wao kukaa chini kwa kukosa Madawati.Lakini pia Mbunge huyo amepeleka madawati zaidi ya 100 kwenye shule mbalimbali ndani ya jimbo lake kulingana na mahitaji ya shule husika.
 Mtendaji wa serikali ya Mtaa wa Shelui(kushoto) wakiwaonesha Wananchi moja ya Dawati zuri na imara sana ambazo Mh.Mwigulu nchemba ametoa kwaajili ya shule ya msingi hapa Shelui.
 Kwenye Mkutano huu wa hadhara.Mh.Mwigulu nchemba alitoa fursa kwa wananchi wake kuuliza maswali mbalimbali yanayohusu mambo ya maendeeleo ndani ya kata na jimbo lake la Iramba.Huyu ni mmoja wa vijana aliyejitokeza kutoa shukrani zake kwa Mbunge wake kwanamna alivyomsaidia kutatua matatizo yake na familia yake.Kijana huyu amewaomba wanashelui kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Mbunge wao kwasababu amekuwa bega kwa bega katika kushughulikia matatizo yao.lakini pia kijana huyu alitumia muda wake kuwaelimisha wananchi wa shelui kuwa na tabia ya kuhoji matumizi ya fedha za Mfuko wa bunge na michango mbalimbali(mapato na matumizi).
Imekuwa ni kawaida kwa wananchi kuogopa kuhoji namna fedha zao zinavyotumika,Hivyo ni muda muafaka sasa kuwabana watendaji wa serikali kutoa mapato na matumizi ya fedha za maendeleo ndani ya kata zao na wilaya kwa ujumla.
 Mh.Aden Rage na Mwigulu Nchemba wakisikiliza ukaribisho wa mwenyekiti wa Tawi wa chama cha mapinduzi(hayupo pichani),
 Wananchi na Mbunge wao hapa Shelui wakimsindikiza kupanda gari.
 Ilikuwa ni furaha kwa Mwigulu nchemba kuzungumza na wananchi wake kuhusu maendeleo anayowafanyia,Picha hii imepigwa wakati anacheza wimbo wa kinyiramba kufurahia namna wananchi walivyojitokeza kwa wingi kumsikiliza kwenye mkutano wake,.
 Huu ni upande mwingine wa wananchi waliofika kusikiliza mkutano wa Mbunge wao Mh.mwigulu nchemba.
 Mh.Mwigulu Nchemba amewasisitizia sana wananchi wa Shelui na Iramba kushiriki kwenye kazi za maendeleo,Kuachana kabisa na kumtegemea Mbunge kufanya kila kitu.Pia amewaomba kuhakikisha wanasimamia kidete miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa ndani ya wilaya yake.Pia amewaomba vijana kujitokeza kwenye chaguzi mbalimbali mwaka ujao kwenye serikali za mitaa,Ameyasema hayo kwa kuzingatia kuwa sehemu kubwa ya wananchi wa sasa ni vijana,hivyoi vijana wana fursa ya kushiriki kwenye kazi za maendeleo kwa wingi sana,na endapo watashiriki kwenye chaguzi watakuwa wamejiwekea mazingira mazuri yakuja kuwa viongozi wakubwa baadae.


Mh.Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mwananchi wake akieleka kwenye jukwaa kwaajili ya kuzungmza na wananchi wake wa kata ya Shelui.

3 comments:

  1. hONGERA SANA KAKA HUU NDIO UWAJIBIKAJI KWA WANANCHI...

    ReplyDelete
  2. Hongera sanaa,Comrade kwa uwajibikaji wa dhati na kutumia nguvu yako binafsi katika kupigania maendeleo ya Watanzania hasa maeneo ya Vijijini ,Sekta za Elimu ,Maji safi,kilimo cha biashara na uwezeshwaji kinaitaji sana jitihada na nguvu zenu nyie wenye jicho la tatu kuyatatua ,tupo pamoja katika kupigania maendeleo na ukuzwaji wa pato la watu wetu ..Hongera sana kwa kasi nzuri ya kukimbizana na mwenendo wa kiuchumi wa dunia yetu

    ReplyDelete
  3. Kazi nzuri Jembe endelea kutekeleza ilani ya chama chako kwa wana Iramba,wewe ndio mwiba wa CHADEMA na lazima uwakae shingoni!

    ReplyDelete