Friday, 22 November 2013

KUVULIWA VYEO ZITTO KABWE"NDANI YA CHADEMA AKILI NDOGO INATWALA AKILI KUBWA"


Kuvuliwa vyeo kwa Zitto Zuberi Kabwe na Dr Kitila Mkumbo kutakuwa na visingio vingi, ukweli ni kwamba "NDANI YA CHADEMA AKILI NDOGO INATAWALA AKILI KUBWA" It is natural kwamba akili ndogo ikitawala akili kubwa,
1) Yatatumika mabavu na nguvu nyingi kuizuia akili kubwa kupanda juu,
2) Zitatafutwa sababu nyingi na visingizio uchwara kuhalalisha kuizima akili kubwa tofauti na vigezo vya hoja kwakuwa akili ndogo haiwezi kuizidi akili kubwa kwa hoja,
3) Hutumika vitisho vingi kuzuia akili kubwa kuchukua hadhi yake
4) Akili ndogo ni rafiki wa akili ndogo mwenzake, hivyo akili ndogo huzungukwa na akili ndogo kwakuwa ushauri wa akili kubwa akili ndogo hushindwa kutumia ama kushindwa kuonesha umiliki mbele za watu. 

Kwenye chadema wenye akili wote wako nje ya uzio wa chemichemi ya mawazo. Pale bungeni watu wanaoweza kufundisha na waliokuwa wakifundisha hata unaibu waziri kivuli hawapati kwakuwa wanatumia akili zaidi badala ya nguvu.
Lakini walioishia kidato cha kwanza, pili, tatu na zero ndio think tanks na ndio majembe ya chadema kwakuwa wanatumia mabavu na manguvu zaidi kuliko akili sawasawa na matakwa mahitaji ya akili ndogo inayoongoza akili kubwa.
Vijana wahitimu wa vyuo wanaopenda siasa waliandikiwa barua kuwazuia kuhutubia mkutano wowote wa hadhara sawasawa na matakwa ya akili ndogo inapotawala akili kubwa. Zito, Kitila, Christowaja, Matiko, Opulukwa, Baregu, Leticia, Selasini, Arfi, Akunay, Naste wengi wao MA holders kwa chadema ni rejects. Ukiwa mwanafamilia au ukoo au kazi au wito maalum wa viongozi ndio utakwepo kwenye list.
I know Zitto tangu tukiwa chuoni, he is a brilliant and consistent politician, namjua Dr Kitila tangu chuoni, he is resourceful. Hivi kosa walilofanya ni kubwa kuliko mchango wao waliofanya kwenye kuwajenga watanzania kuwaamini vijana kwenye siasa? Je kosa lao ni kubwa kuliko mchango wao unavyohitajika? Vijana tuko kazini na wakati huohuo tuko mafunzoni.
Sio adhabu nzuri ya kuwafukuza ama kuwaondoa kwenye fursa ya kujifunza zaidi

16 comments:

  1. hapa umenena jambo la mahana sana nahisi cdm wamechemka big time na hii itawagharimu

    ReplyDelete
  2. Mwigulu,hii blog ina muonekano usiovutia kabisa plus hakuna weledi kwenye maandishi kiasi hata kuruka mstari kati ya paragraph na paragraph inashindikana, kwanini usitafute mtu adesign website au blog nzuri kwa ajili yako?, ni maoni tu usirushe mawe.

    ReplyDelete
  3. kaka,haya masifa ulowamwagia hawa jamaa mbona hatukuskia ukiwasifu kabla ya tukio hili? au mnawapampu ili wajitutumue na wajihisi wenye mvuto sana kule cdm? wakifuata mawazo yako,watajikuta wanatimuliwa kabisaa na waanzekulia kama alivyolia Kafulila akidai anawalilia wapiga kura wake!

    ReplyDelete
  4. Mheshimiwa sidhani kama kuwa ma masters ndio kigezo cha kuwa kiongozi mzuri.Hapo zamani nchi hii ilikuwa na viongozi waadilifu sana na hawakuwa na elimu kubwa,na mambo yalienda lakini baada ya hao wenye masters kuingia ndani ndipo tunaposhudia uozo na wa kutisha.Kwa maoni yangu mheshimiwa uongozi ni kipaji na uongozi hausomewi,elimu inakusaidia kuwa na uwezo mkubwa wa kupambanuwa mambo katika jamii inayokuzunguka!

    ReplyDelete
  5. Kukujibu ni kujidhalilisha tu!

    ReplyDelete
  6. Kaka waachie wananchadema tu mabo yao

    ReplyDelete
  7. Sisi wakazi wa Kigoma tunaifahamu sana historia ya hii SACCOS (chadema) kumbukeni sababu za
    Kuondoka kwa Dr Aman Walid Kabur, kufukuzwa kwa Mh David Kafulila na hatimae Mh zitto Kabwe.
    Hawa wote ni wana Kigoma lakini leo hatuna sababu za kuumiza vichwa kutafakari nini kiini cha haya kwasababu Chadema wamejikaanga kwa mafuta yao wenyewe asubuhi na mapemaaa.KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

    ReplyDelete
  8. Sio adhabu nzuri ya kuwafukuza ama kuwaondoa kwenye fursa ya kujifunza zaidi , Nimeupenda mstari wa mwisho.

    ReplyDelete
  9. Sio adhabu nzuri ya kuwafukuza ama kuwaondoa kwenye fursa ya kujifunza zaidi , Nimeupenda mstari wa mwisho.

    ReplyDelete
  10. who are you to write this??

    ReplyDelete
  11. Una machungu sana na Chadema? Unaipenda au ni unafiki?

    Kwa kuwa ccm haina ubavu wa kufanya maamuzi, sishangai unaposhangaa juu ya maamuzi ya cdm kwani hujui maana ya kufanya maanuzi.

    ReplyDelete
  12. kweli hata hizi comment ni akili ndogo tupu!kumbe ndo maana nchi hii inaendeshwa kimabavu kumbe ni akili ndogo!na kila akili ndogo inamdogo wake,ww hao uliowaona na akili kubwa wamekutana na kubwa kuliko!kama wameonewa watakata rufaa!hata mwenye akili akikosea lazima aadhibiwe!ccm ndo wanawaogopa kuadhibiana ndo maana nchi imekua kama demu wa mtungo!

    ReplyDelete
  13. Ni kweli Kiongozi, nimekusoma maana hawa CHADEMA wanakurupuka kuchukua maamuzi badala ya kuchunguza na kufikia hatua ya mwisho ni akina nani intellectual or not, maana pale ni ukanda tu, kama haujabahatika kuzaliwa kaskazini imekula kwako hata kama unahoja nzuri kiasi gani,

    ReplyDelete
  14. ama kweli umeumia sana mbona unasahaukuwa unahusika

    ReplyDelete
  15. homgera kk umeona mbali, usemayo ni kweli @AKILI NDOGO DAIMA UFUKUZA AKILI KUBWA KWA NJIA YEYOTE ILE"

    ReplyDelete
  16. homgera kk umeona mbali, usemayo ni kweli @AKILI NDOGO DAIMA UFUKUZA AKILI KUBWA KWA NJIA YEYOTE ILE"

    ReplyDelete