Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi katika picha tofauti akizungumza na wananchi wa Tanga Mjini hii leo kwenye Viwanja vya Tangamano wakati wa Mkutano wa kuomba kura za Urais,Ubunge na Udiwani kwaajili ya kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo mapema October 25.2015.
Magufuli amewaahidi Wananchi wa Tanga kuwa atarejesha Viwanda na atahakikisha Tanga Unakuwa Mkoa wa Viwanda kama zamani.Mbali zaidi amesema amenuia kuhakikisha Taifa linabadilika kwenye Utendaji wakazi,Utoaji wa huduma na Uimarishwaji wa Uchumi ilikutoa fursa sawa kwa Watanzania wote bila kujali vyama,kabila na dini zao waweze kunufaika na keki ya Taifa.Hisia za Wanafunzi wa elimu ya Juu wanaosoma Mkoani Tanga,Wanaimani na Magufuli na wanampigania awezekushinda nafasi ya Urais.Sehemu ya Maelfu ya Wananchi wa Tanga wakifuatilia Mkutano wa Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi Mh.J.J.P.Magufuli hii leo.Hisia za Wananchi wa Tanga Mjini wa Rais Mtarajiwa Mh.J.Magufuli.Kada Mtiifu wa chama cha Mapinduzi Mh.Mwigulu Nchemba akiwasihi Wananchi wa Tanga kuepuka wadanganyifu wakati huu wa Uchaguzi,Amesisitiza wagombea Urais wote ni Zao la CCM,Hivyo wapo waliokimbia CCM na kuhamia Upinzani ili wapate Madaraka na sio kwaajili ya dhamira ya dhati ya kuwatumikia Watanzania.Mwigulu ameenda mbali zai kwa kusema CCM ndio Chama kilichosimamisha Mgombea anayepinga Rushwa kwa Vitendo jambo linalomtofautisha na Wagombea wengine ambao wananuka Rushwa katika maisha yao yote.Mh.January Makamba akizungumza na Wananchi wa Tanga juu ya Umuhimu wao wa kuichagua CCM kuongoza kwa awamu ya Tano,Makamba amesisitiza vijana kufanya maamuzi ya Taifa lao bila Ushabiki ,bali wazingatie ubora wa kiongozi na rekodi zao za utendaji kazi.Hazina ya CCM ya miaka ijayo ikijadiliana jambo(January makamba,Ummy Mwalimu na Mwigulu Nchemba)Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mh.Yusuph Makamba.Sehemu ya Wananchi wakifuatilia Mkutano wa kampeni wa Chama cha Mapinduzi viwanja vya Tangamano.Mh.J.P.Magufuli akijadiliana jambo na aliyekuwa Naibu katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mh.Mwigulu Nchemba.
Picha na Sanga Jr.
No comments:
Post a Comment