Mh
James Mbatia(MB) Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi akitoa neno la Shukrani kwa
Watanzania na Wananchi wote waliojitokeza kufanikisha Shughuli ya
Mazishi ya Marehemu Dr.Mvungi.Katika Hotuba yake Mh.Mbatia ameomba na
kusisitiza sana serikali iimarishe ulinzi kwa gharama yeyote
ile,Serikali ichukue hatua madhubuti kupambana na watu wanaojihususisha
na vitendo vya kinyama kama hiki alichofanyiwa Marehemu Mvungi cha
kuvamiwa na kukatwa Mapanga na kupelekea kifo chake.
Watoto
wa Marehemu Dr.Edmund Sengondo Mvungi wakitoa neno la shukrani kwa
waombolezaji wote walojitokeza kwenye mazishi ya Baba yao,pamoja na
namna serikali na viongozi wa NCCR walivyopambana kuokoa Uhai wa Baba
yao bila Mafanikio.Kubwa Watoto wameahidi kuwa Watasoma sana kama Baba
yao alivyosoma na kuwa msaada kwa taifa.
Mh.Mwigulu
Nchemba(MB) na Naibu katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara akitoa shukrani
za rambirambi akimuwakilisha Katibu Mkuu wa CCM Kanali Mstaafu Abrahaman
Kinana,Katika Salamu zake,Mwigulu Nchemba amewasihi waombolezaji na
watanzania kukemea na kuombea Taifa lisipatwe zaidi na huyu pepo wa
mauaji anayeendelea kulikumba Taifa.Amesisitiza kuwa Serikali haiwezi
kuwa sehemu yote ya nchi hii kwa muda wote,kikuwa ni ushirikiano wa
Wananchi na vyombo vya Usalama kufichua mitandano hii ya unyama na
mauaji.Mwigulu amesisitiza kuwa Taifa linapatwa na mikasa hii kwasababu
watu hawana hofu ya Mungu,hivyo ni wakati wa kuamka kama Taifa na
kushikamana kuombea taifa letu na kufichua maovu.
Mh.Steven
Masatu Wassira akitoa salamu za rambirambi kutoka Ofisi ya Rais,ambapo
Mh.Wassira alisema Rais kikwete anatoa pole sana kwa familia na
Watanzania wote kwa tukio hili ya kuondokewa na mtu muhimu sana kwa nchi
yetu hasa kwa Mchakato mzima wa Mabadiriko ya katiba unaoendelea.
Mh.waziri
Mkuu Mizengo Peter Pinda akitoa Salamu za rambirambi kwa familia ya
Marehemu Dr.Sengondo Mvungi,Kubwa alilozungumza Mh.Pinda ni kuwaomba
watanzania kujiepusha na matendo maovu haya ya kuua watu wasio na
hatia.Ameahidi serikali itafanya kazi yake kuhakikisha wahusika
wanafikishwa sehemu husika na wanapata kuvuna dhambi walioipanda.Pia
amewasihi Watanzania kumuombea Marehemu Mvungi huko aliko apokelewe na
Bwana.
Waziri
Mkuu Mstaafu Jaji Warioba akitoa Salamu za rambirambi kwa waombolezaji
na kumuelezea namna Marehemu Edmund Sengondo Mvungi alivyokuwa na msaada
mkubwa kwneye mchakato wa katiba Mpya,Namna Mvungi alivyotanguliza
Utaifa mbele na kauchana na ushabiki wa Chama.Mh.Warioba amesema
anamuomba sana mungu waikamilishe kazi waliyotumwa na taifa hili(Katiba
mpya) kwa amani licha ya kupata pigo kubwa la kuondokewa na kiungo
muhimu sana kwenye mchakato mzima wa mabadiriko ya Katiba.
Askofu
kwa Kaskazini akilisha neno la Mungu waombolezaji wakati wa Ibada ya
kuuga Mwili wa Marehemu Sengondo Mvungi.Askofu ameiomba sana serikali na
Watanzania kuacha kabisa kufanyiana unyama wa namna alivyofanyiwa
Mvungi kwakuwa mshahara wa dhambi niMauti.Na zaidi amesisitiza kuwa kila
kiongozi,mwanasiasa na mtanzani mmojammoja ajitazame njia zake kwa
namna anavyoishi na anavyolisaidia Taifa lake lisipatwe nda hii taibia
ya watu kuuana na mmomonyoko wa maadili kwa vijana wetu.
Mh.Mwigulu
Nchemba akikabidhi rambirambi ya CHAMA CHA MAPINDUZI kwa mmoja wa
wanafamilia wa Marehemu Edmund Sengondo Mvungi mbele ya
waombolezaji.Rambirambi imetolewa na chama cha mapinduzi.
Baba Askofu akiweka Shada la Maua kwenye jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Dr.Edmund Sengondo Mvungi.
Mh.Maghembe(kushoto)
Mbunge wa Jimbo la Mwanga jimbo alilozaliwa Marehemu Mvungi akisikiliza
kwa makini mafundisho ya Baba Askofu,.Huku(Kulia) Mh.Mwigulu Nchemba
akiwa na uso wa huzuni kwa kumpoteza msomi mwenzake,Mwanasiasa Mwenzake
Marehemu Edmund Sengondo Mvungi.
Mh.Mwigulu Nchemba Mbunge wa Iramba Magharibi na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara akitoa Heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Dr.Edmund Sengondo Adrian Mvungi wakati wa Ibada ya mazishi iliyofanyika Parish ya Kisangara Juu wilaya ya Mwanga.
R.I.P DR.EDMUND SENGONDO ADRIAN MVUNGI
Nikiwa mmoja wapo wa wana Kilimanjaro, nawashukuru watu wote na serikali ya ccm kwa jinsi mlivyojitokea kupitia waziri Mkuu, wamaziri wote, tume ya katiba na Mhe. Mwigulu Mnchemba aliyekuwa pamoja nasi kwenye msiba huo Vujini, Kisangara Juu.. Mch. Palemo Massawe
ReplyDeleteNIwashukuru wote hasa Mhe. Mwigulu Mchemba kwa kazi kubwa waliyofanya kusaidia kumpumzisha ndugu yetu hayat, Dr. Mvungi
ReplyDeleteMh Kiongozi wa Upizani Kwenye Bunge la Jamuhuri ya Tanzania alikuwepo? kama alikuwepo mbona picha zake hazionekani; na alizungumza kabla yako; na kama wewe ndio ulikuwa mpiga picha basi ungempiga;Nisingeshangaa kutokuiona picha yako kama wewe ndio ulikuwa mpiga picha;Naomba maelezo'Au uchama nao;ulikuwa mbele kuliko utanzania; au kombati zake hazikuvutia kumpiga picha?
ReplyDelete