


Waziri wa Nishati na Madini akiwa na Mwenyeji wake Mh:Mwigulu Nchemba wakisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Kaselya.
Mkuu
wa Wilaya ya Iramba Mh:Yahya Nawanda(kulia) akibadilishana Mawazo na
Mbunge wa Iramba Mh:Mwigulu Nchemba hii leo kwenye Mkutano na Wananchi
wa Kaselya kuwaelezea Fursa waliyonayo kwenye Umeme walioingiziwa
Kijijini Kwao.
Mh:Mwigulu
Nchemba akifurahia na Wananchi Wake wa Kijiji cha Kaselya mara baada ya
Kupokea Umeme na Kuwaelimisha Wananchi faida za Umeme huo.















Waziri
wa Nishati na Madini Mh:Sospeter Mhongo hii leo akiwa na Mwenyeji wake
Mbunge wa Iramba Magharibi Mh:Mwigulu Nchemba Wametembelea Utekelezaji
wa Mradi wa Umeme Mkoani Singida kwa Wilaya ya Iramba.
Wilaya
ya Iramba (JImbo la Mh:Mwigulu Nchemba) Mradi wa Umeme Vijijini
Umevifikia Vijiji 43 katika Jimbo lote la Iramba,Mh:Mhongo
amesema,Serikali imetenga Bilioni 31.9 kwa Mkoa wa Singida kuhakikisha
Umeme unasambazwa sehemu Kubwa ya Vijiji ilikufungua Milango ya Kukua
Uchumi na hatimaye Kuondokana na Umaskini.
Kwa
Wananchi Watanufaika Zaidi na Mradi huo kwasababu Uunganishaji wa Umeme
kwenye Makazi ni kwa Bei Nafuu sana,Mwananchi atatakiwa Kuchangia
Tsh;27000(Elfu Ishirini na Saba tu) Kuunganishiwa Umeme Nyumbani Kwake
tofauti na Kipindi cha Nyuma Umeme ulikuwa Unaunganishwa kwa Shilingi
Laki nne na baadae Laki moja na Sabini.Hiyo 27000/= itakubalika tu
endapo Mwananchi ataunganisha Umeme wakati Mkandarasi bado anaendelea na
Ukamilishaji wa Mradi.
Akizungumza
na Wananchi wa Mgongo,Mh:Mhongo amesema"Serikali ya CCM imedhamiria
kufikisha Umeme kila Kona ya Nchi hii,Gesi tunayo ya Kutufanya tufikishe
Umeme popote pale,Wananchi manaombwa Kuonesha Umoja wenu katika hatua
hii ya MATOKEO MAKUBWA SASA ili Uchumi wa Nchi yetu ufikie pale
tunapotakiwa Kufika.
Vilevile
Mbunge wa Iramba Mh:Mwigulu Nchemba ametoa rai kwa Wananchi Wake
kuchangamkia Fursa hiyo ya Kuunganishiwa Umeme kwa bei nafuu,Umeme wa
bei nafuu Ulikuwa ni Historia kwa Nchi hii lakini sasa Umepatikana.Hivyo
amewaomba Wananchi wa Vijiji Vyote 43 vinavyopitiwa na Mradi wa Umeme
huo kujipanga Kutumia Umeme kwaajili ya Kuinua Uchumi wao.
"Mimi
kazi Mkataba wangu na Nyie Wananchi nia Kuwaletea Maendeleo tu,Hivyo
nitaendelea kuwaletea Maendeleo kadri ya Uwezo Wangu,Tuungane Mkono
tufute Umaskini Kwa Wananchi wa Iramba" Mwigulu.
Vijiji Vilivyopata Kunufaika na Mradi huo ni,Mbelekesye,Mgongo,Kiselya,Mtoa,Kibaya(Endelea Ku-refresh page tunaandika Vijiji Vyote).
Picha/Maelezo na Sanga Festo
No comments:
Post a Comment