Thursday 7 November 2013

SOMO KWA WATANZANIA,KUVAMIWA KWA GOLD CREST HOTEL NA MAGAIDI(POLISI) HII LEO

Ikiwa ni mwezi mmoja na siku kadhaa zimepita tangu kutokea kwa tukio la kigaidi la uvamizi wa maduka ya Westgate mjini Nairobi yaliyofanywa na kundi la wanamgambo wa al-Shabaab, asubuhi ya leo ya Novemba 7 2013, mamlaka za usalama Mkoani Mwanza zimefanya uvamizi kwenye hoteli ya Gold Crest ya jijini Mwanza.
Uvamizi huo ambao kwa taarifa za awali kutoka katika vyanzo vyetu lilikuwa ni la jaribio kuona uwezo na namna ya wananchi na jamii kwa ujumla wanavyoweza kukabiliana na matukio ya aina hiyo.
Hata hivyo tukio hilo lililochukua muda wa saa nzima limeibua takaruki kwa wananchi waliokuwa ndani ya hoteli na nje ya hoteli hiyo jambo lililopelekea umati wa watu wengi kukusanyika kwa lengo la kujua nini kinachoendelea.
Hakika kwa utamaduni huu wa watanzania kukimbilia kwenye eneo la tukio badala ya kukimbia sehemu salama kuna hatari ya watu wengi kupoteza maisha kama tukio kama hili likitokea katika mazingira ya uhalisia (tunaomba manani atuepushe na mabalaa ya namna hii). Tazama picha zote za tukio hili lakini nitoe angaliazo tu kuwa TUKIO HILI NI LA MAJARIBIO NA LIMEFANYWA KWA KUSHTUKIZA.

1 comment:

  1. ARBOGAST KIWALLE7 November 2013 at 03:54

    Kwa kweli ni hatari sana kwa Watanzani endapo kwa bahati mbaya ikatokea watu wengi watapoteza maisha,Naomba vyombo vya Habari haswa TBC IWE NA KIPINDI MAALUMU HATA DK 15 KWA AJILI YA KUTOA ELIMU

    ReplyDelete