











Katika ziara yake kwenye kambi ya wakimbizi ya Katumba na Shimano,Mwigulu Nchemba amezungumza na wakimbizi hao ambao wale wa Katumba walipewa Uraia mwaka 2009 na wa Shimano bado hawajapewa Uraia.Akizungumza nao katika hali ya kusikitisha,kuna baadhi ya watu tumewapa Uraia lakini matendo yao yanachafua hali ya usalama wetu,miongoni mwenu kunawanaojihusisha na wizi,uhalifu wa kutumia silaha,kuhifadhi waovu na kufanya vitendo vya kibaguzi kwa misingi ya maeneo mnayotoka.
Mbaya zaidi,kunawakimbi waliopewa uraia hapa nchi wanawatenga watanzania kwamba hawawezi kushirikiana nao.Natoa onyo kwa wote wanaofanya vitendo vya kibaguzi na kihalifu,Tanzania inaishi kwenye misingi ya Umoja,mshikamano na Ushirikiano wa hali ya juu bila kubaguana.Hivyo hatutakuwa tayari kwa watu wachache kuleta tabia mbovu ambazo hatujawahi kuziishi na tunaomba kila siku tusije kuziishi."anasema mwigulu.
Picha/Maelezo na Sanga Festo Jr.
No comments:
Post a Comment