Dk. Sengondo Mvungi akiwa amepakiwa katika ndege leo |
DAR ES SALAAM, Tanzania
Mjumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dk. Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata
matibabu katika Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) baada ya kuumizwa
vibaya na majambazi, amesafirishwa leoi, Novemba 7, 2013) saa 5:45
asubuhi kwenda nchini Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
Taarifa
iliyotolewa na Tume hiyo, imesema, akiwa nchini Afrika Kusini, Dk.
Mvungi atapata matibabu katika Hospital ya Milpark iliyopo jijiniJ ohannesburg.
"Itakumbukwa
kuwa Dk. Mvungi alivamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya ya Kinondoni
jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani usiku wa
kuamkia sJumapili, Novemba 3, 2013. Tukio hilo la uvamizi linaendelea
kuchunguzwa na vyombo vya ulinzi na usalama nchini", ilisema taarifa
hiyo.
Imesema
tangu siku alipojeruhiwa, Dk. Mvungi alikuwa akipata matibabu katika
Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI). Hata hivyo, Madaktari waliokuwa
wakimtibu MOI, walishauri afanyiwe uchunguzi na matibabu zaidi.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, Dk. Mvungi ameondoka na ndege ya kukodi ya
Shirika la Ndege la Flightlink na ameambatana na Dk. Mugisha Clement
Mazoko kutoka MOI, Muuguzi Bi. Juliana Moshi, na mtoto wa kaka yake Bw.
Deogratias Mwarabu NA KWAMBA Serikali inagharamia gharama zote za
matibabu ya Dk. Mvungi.
Tume
imewaomba wananchi wote waendelee kumuombea kwa Mungu Dk. Mvungi ili
aweze kurejea katika hali yake ya kawaida na hatimaye kuendelea majukumu
yake.
No comments:
Post a Comment