Friday, 22 November 2013

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYA YA NYASA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya jinsi ya kutumia vifaa vya maabara katika kufanikisha kutambua kemikali kutoka kwa wanafunzi wa kidato cha nne Erasto Ndumba na Stella Hyera wa shule ya sekondari ya Kata ya Mtakatifu Paul kata ya Liuli wilaya ya Nyasa
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi nyumba za madaktari zilizochini ya mradi wa Taasisi Benjamini Mkapa katika kituo cha afya  Mkili kata Liundi wilayani Nyasa.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishauri jambo kabla ya kuvuka mtu Ruhuhu kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Mwenyekiti wa CCM Ndugu Oddo Mwisho.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Ndugu Ernest Kahindi wakivuka kwa mtumbwi kuelekea kijiji cha Kipingu wilaya ya Ludewa.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimu wakazi wa kijiji cha Kipingu wilayani Ludewa, Kijiji hicho kipo mpakani wa mkoa wa Ruvuma na Njombe. Katibu Mkuu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa kata Kipingu kijiji cha  Kipingu wilaya ya Ludewa ambapo aliwaambia ahadi ya kujengwa kwa daraja la mto Ruhuhu, uzalishaji wa umeme utakotosheleza mahitaji ya  wilaya ya Nyasa na Ludewa pamoja na mradi wa umwagiliaji.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipungia wananchi wakati akirejea kijiji cha Lituhi kwa Mtumbwi  baada ya kutoka kuwasalimu wakazi wa kijiji cha Kipingu wilayani Ludewa,wengine pichani ni Dk.Asha-Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na kikundi cha akina mama wakulima wa mpunga na mboga mboga wa kijiji cha Lituhi katika viwanja vya Lituhi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma Verena Shumbusho wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa  Mbinga Magharibi Kapteni John Komba wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mikutano Lituhi ambapo vijana 12 kutoka vijiji mbali mbali walipewa mabati kwa ajili ya kuezeka nyumba zao.
 Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni John Komba akimtambulisha Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kama Ndugu yake wa karibu kwani mafanikio yake yametokana na mchango mkubwa wa Marehemu Mzee Nnauye ,Pia Komba alimuelezea Kinana kama mmoja wa walimu wake wazuri wa masomo ya kijeshi pamoja na siasa.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akionyesha kadi za wanachama  wa Chadema waliorudi CCM baada ya chama chao kuanza kuparanganyika,mkutano huo uliofanyika kwenye viwanja vya Lituhi ambapo wanachama zaidi ya 400 wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanachama waliojiunga na CCM kutoka vyama vya upinzani.

No comments:

Post a Comment