![]() |
Mh.Mwigulu
Nchemba akiwa na uso wa Furaha mara baada ya kuwasili kwenye Mkutano
wa Hadhara kijiji cha Kibaya kata ya Ndago mapema hii leo
Tar.11/11/2013 |




Picha ni mapokezi ya Mh.Mwigulu Nchemba kijiji cha Lunzinzi kata ya Ndago wakati wa mkutano wa hadhara hii leo.


Na Ibrahim Makunda.
Mbunge wa Iramba Mgharibi na Naibu katibu Mkuu wa CCM leo amefanya ziara ya kuzungukia jimbo lake upande wa kata ya Ndago kwa lengo la kukutana na wananchi wake kujadiliana kuhusu mambo ya maendeleo na kutoa mrejesho wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayofanyika ndani ya kata ya Ndago.Mwigulu Nchemba amefanya mikutano mitatu katika vijiji vya Kibaya,Songa Mbele na Lunzinzi ndani ya kata ya Ndago,katika mikutano hiyo Mh.Mwigulu Nchemba alizungumza na wananchi wake kuhusu mpango wa kusambaza umeme Kuanzia Ndago kupita barabara ya Vumbi kueleka kaskazini hadi Mashariki mwa jimbo hilo la Iramba kuelekea Singida Mjini.
Mpango wa kusambaza umeme huo umeshaanza na baadhi ya vijiji umeshaanza kuwaka, Pia Mbunge huyo amezungumza na wananchi wa kata ya Ndago kuhusu barabara ambayo imekamilika na inapitika kiurahisi kutoka Ndago kwenda singida Mjini,lakini pia ametoa mrejesho wa Ujenzi wa vituo vya Afya kila kijiji cha kata ya Ndago na namna alivyofanikisha kupatikana kwa Magari mawili kwaajili ya Hospitali ya Ndago kwaajili ya kutoa huduma kata nzima na jimboni hapo.
Katika hali ya kuonesha namna Mbunge huyo yupo na Wananchi bega kwa bega amechangia Cash ujenzi wa Vituo kadhaa vya huduma za Afya,Pia amechangia papo kwa papo vikundi vya Uimbaji na vyaasili pamoja na timu za Mipira kwaajili ya kuimarisha umoja miongoni mwa Wananchi wake.
Kwenye sekta ya Elimu Mh.Mwigulu Nchemba amesambaza vitabu vyenye thamani ya Milioni 16 za Kitanzania katika kata nzima ya Ndago,huku akichangia madawati kila shule yenye tatizo la Madawati.
Pamoja na hayo,Mbunge huyo ametoa nafasi kwa Wananchi wake kuuliza maswali ya papo kwa papo na kujibiwa vyema na yeye mwenyewe akishirikiana na viongozi wa serikali aliombatana nao hususani sekta ya kilimo na Ufuatiliaji wa Mapato na Matumizi ya serikali za vijiji.
Pia amewasihi sana wananchi wake kujishughulisha na kazi za kilimo kuhakikisha wanaondokana na njaa,amewataka Wananchi kujiandaa na kilimo msimu huu wa mvua unapoanza,pembejeo zimeshafika wilayani na kila mmoja anahaki ya kupata.Hivyo fursa pekee ya kuondona na njaa na vyakula vya misaada ni kujikita kwenye uzalishaji kupitia kilimo na kaucha kuharibu vyanzo asili hasa ukataji ovyo wa misitu.
Mwisho kabisa Mh.Mwigulu Nchemba aliomba Wananchi wa Ndago kudumisha amani na mshikamano huku akiwambia kuwa Kinachomuunganisha yeye na WanaIramba ni maendeleo tu,mengine yanafuata.Hivyo basi WanaIramba wanapaswa kuhakikisha wanambana pale ambapo hajatimiza,pia kuibana timu yake ya kazi ndani ya jimbo kuhakikisha shughuli zote za maendeleo zinafanyika kwa wakati na kwa ufanisi.
naona ulikua nyumbani kwetu kabisa,hongera sana.
ReplyDelete