Thursday 14 November 2013

"UCHAGUZI MWAKA 2015,KUNDI LANGU NI CCM"--MWIGULU NCHEMBA

Watanzania,
Nimelazimika kusema machache kutoa ufafanuzi kufuatia uzi wa Mwita Maranya na wengine wenye fikra hizo (Uzi huu hapa>>http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/553018-mwigulu-nchemba-kumlima-barua-kinana.html). Mwita ama kwa kutokujua historia yangu na uzito wa nafasi niliyonayo amenipa ufusia wa mgombea arais au kundi la mgombea. Kwa historia yangu na kwa nafasi yangu ndani ya chama huu sio muda wa kuwa na kundi. KUNDI LANGU NI CCM. NITAWAUNGA MKONO WAGOMBEA WA NGAZI ZOTE WATAKAOKABIDHIWA JUKUMU LA KUPEPERUSHA BENDERA YA CCM 2015 KWA MJIBU WA KATIBA NA KANUNI ZA UCHAGUZI NDANI YA CCM.

Mosi, historia yangu kwenye siasa, mimi sio matokeo ya jitihada za kundi lolote kufika hapa. Niligombea ubunge nikiwa sijulikani na kundi lolote na wala sikutengenezwa na kundi lolote.Ungekuwa wakati wa kutafuta kundi ungekuwa huo maana nilikwenda kugombea nikiwa sina baisikeli, pikipiki wala gari. Ungekosa sifa zote kuhusu mimi, moja tu ungepewa na wanaccm ni kwamba mimi sina kundi na sitokani na makundi yanayokinzana, sina chuki na kundi lolote na wala siegemei kundi lolote. Hivyo hivyo nilishinda kwa kishindo uchaguzi ndani ya chama moja ya sababu nikutokuwa na ugomvi wala chuki na wanaccm na sina sababu na sioni faida ya kuingia kwenye makundi katika ngazi hii na muda huu. AM THE ACTOR AND DIRECTOR OF MY OWN IN POLITICS.

Pili kwa nafasi yangu mimi ni mkuu wa utumishi na utawala. Nimekuwa msiri wa mbele kuzuia watumishi wote na viongozi wa kuchaguliwa kutoingia kwenye makundi ya wagombea mpaka pale chama kitakapo watangaza kupitia NEC ya CCM. Nimetoa maelekezo hayo mikoani na wilayani kwa barua. Haiwezekani nitoe maelekezo kuwazuia wenzangu halafu mimi niwe kwenye kundi lililowazuia wenzangu. Ndio maana sijawahi shiriki kikao, mazungumzo yeyote ya kundi la mgombea, wakala wa mgombea au mgombea.

Tatu, kwa nafasi yangu naingia vikao vyote vya maamuzi ya chama vitakavyowajadili wagombea kwa mujibu wa katiba. Natakiwa kuwatendea haki wagombea wote. Sipaswi kuwa na upande katika mazingira hayo kwani huwezikutenda haki ukiwa nawe ni mjumbe wa vikao huku una mgombea. Nani atawatetea au kuwatendea haki wengine wasiokuwa 'wakwako' kiongozi ukiingia kwenye makundi.

Nne kuwa na kundi kunakusabisha kuchukiwa na wanaccm wenye makundi yao au wagombea wao kisirisiri. Mimi naungwa mkono na wana ccm wote kwa sifa hiyo ya kujenga chama na kuwaunganisha wanaccm. MAKUNDI YOTE WANAONA NAWATENDEA HAKI PUNDE KUNA KITU KINAHITAJI UAMZI.

Ukiwauliza wanaccm wakutajie watu watatu ambao wana imani nao wanaoweza kuwaunganisha na kuwapa ushindi nami nipo.

Nikuulize swali Mwita, umekiri mwenyewe kuwa wanaccm wanamatumaini makubwa namimi ya kuwavusha, umekiri pia kuwa napendwa na vijana. Ila umenipa ufuasi kwenye makundi ya wagombea, ULIWAHI KUNIULIZA BINAFSI NIKAKWAMBIA SIGOMBEI HATA UHANGAIKE KUBASHIRI KUWA MIKI NIMFUASI WA KUNDI FULANI.? MIMI NI KIUNGO NA KIONGOZI WA CCM NA MAKUNDI YOTE NDANI YA CCM.

CHAMA CHETU NI CHAMA CHA UTARATIBU NA MIMI NDIO MSIMAMIZI MKUU WA UTARATIBU NDANI YA CHAMA. KUNDI LANGU NI CCM.
Soma zaidi>>http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/553466-urais-2015-kundi-langu-ni-ccm.html

1 comment:

  1. Mkuu Hongera sana, kwa maamuzi hayo na pia kwa kuelewa majukumu yako katika kukijenga chama chetu. Endelea hivyo hivyo ili chama chetu kisirudi nyuma. MUNGU awe pamoja nawe.

    ReplyDelete