Kadhalika, Mkurugenzi wa Mawasiliano
Ikulu, Salva Rweyemamu alithibitisha kuwa Rais Kikwete atalihutubia
Bunge, Alhamisi... "Nathibitisha ni kweli, ila kwa taarifa nyingine
watafuteni watendaji wa Bunge, kama Katibu wa Bunge nadhani wana taarifa
zaidi."
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah
alithibitisha jana katika Viwanja vya Bunge Dodoma kuwapo kwa ratiba ya
Rais Kikwete kulihutubia Bunge na kwamba taarifa rasmi ingetolewa jana
jioni kwa wabunge.
"Ni kweli Rais anatarajiwa kuja kulihutubia Bunge na leo (jana) jioni, tutatoa taarifa rasmi bungeni," alisema Dk Kashililah.
Mara ya mwisho Rais Kikwete
alilihutubia Bunge wakati akifungua rasmi Bunge la Kumi, Novemba 18,
2010 alipoeleza vipaumbele vya Serikali yake katika awamu ya pili ya
uongozi wake. Rais Kikwete analihutubia Bunge wakati likisubiri kujadili
mapendekezo ya marekebisho katika Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba ya 2013 ambayo ilipitishwa katika mkutano uliopita.
Tayari Muswada wa Marekebisho
unaopendekezwa umewasilishwa katika Ofisi ya Katibu wa Bunge chini ya
hati ya dharura na leo utajadiliwa katika Kikao cha Kamati ya Uongozi
ili kupata kibali cha kuingizwa ndani ya Kamati ya Katiba, Sheria na
Utawala na baadaye Bungeni.
Dk Kashililah alisema amepokea muswada
huo na kwamba uamuzi wa lini utafikishwa bungeni utafanywa na Kamati ya
Uongozi ya Bunge ambayo itakutana na leo.
Kamati hiyo ndiyo yenye mamlaka ya
kuifanyia marekebisho ratiba ya vikao vya Bunge na kuruhusu mambo
yanayopaswa kuingizwa bungeni kujadiliwa.
Muswada huo ni matokeo ya majadiliano
baina ya Serikali kwa upande mmoja na vyama vya siasa vyenye wabunge
chini ya uratibu wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kwa upande
mwingine, baada ya vyama vya siasa kutoridhishwa na muswada ulipitishwa
katika mkutano wa Bunge uliopita.
Itakumbukwa kwamba wabunge wa vyama
vya upinzani vya Chadema, NCCR Mageuzi na CUF walisusia shughuli za
mchakato wa kupitishwa kwa marekebisho ya sheria hiyo bungeni, hivyo
kutoa fursa kwa wabunge wa CCM kufanya watakavyo kisha kupitisha sheria
hiyo.
Baada ya kupitishwa huko, vyama hivyo
viliendesha kampeni ya kuitisha maandamano nchi nzima, lakini kabla
hayajafanyika Rais Kikwete aliwaalika viongozi wake katika meza ya
majadiliano, mchakato ambao umezaa mabadiliko yanayokusudiwa kuingizwa
bungeni wiki hii.
Katika mazingira hayo kumekuwa na hofu
kwamba huenda wabunge hasa wa CCM wakatumia wingi wao kukwamisha
mabadiliko yanayopendekezwa kutokana na kukasirishwa kwao na kile
kilichoonekana kuwa ni Rais Kikwete kuwasikiliza wapinzani.
Hiyo inaweza kuwa ndiyo sababu kubwa
ya Rais Kikwete kuamua kulihutubia Bunge kwa lengo la kujenga msingi wa
maridhiano katika mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya kama ambavyo
amekuwa akisisitiza mara kwa mara.
Wednesday, 6 November 2013
TAARIFA :RAIS KIKWETE KUHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,HAPO KESHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment