Wednesday, 6 November 2013

MKOA WA MBEYA WASHINDWA KUFIKIA MALENGO MWAKA WA FEDHA 2012/2013

Mwenyekiti wa kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro.
 Awali akifungua Mkutano huo Kandoro alisema lengo na madhumuni ya kikao hicho ni kujadili bajeti ya Mkoa kwa mwaka wa fedha 2012/2013 na Mwaka wa fedha 2013/ 2014 sambamba na kuangalia utekelezaji wake na changamoto zilizojitokeza katika ukamilishaji wa miradi kwa kila Halmashauri.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja ambaye pia ni katibu wa kikao hicho alisema changamoto zilizojitokeza ni pamoja na kuchelewa kutolewa kwa fedha za maendeleo na wakati mwingine kutolewa kidogo kidogo hali hiyo mhusababisha kuchelewa kuanza kutekeleza kwa baadhi ya miradi husika.



KATIKA utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa Fedha wa 2012/2013, Mkoa wa Mbeya umeshindwa kukidhi mahitaji kutokana na kukabiliana na changamoto mbali mbali ikiwemo ucheleweshaji wa fedha kutoka Hazina.
Hayo yalibainishwa katika Kikao cha Ushauri cha Mkoa wa Mbeya (RCC) kilichofanyika hivi karibuni`katika ukumbi wa Mikutano wa Mkapa uliopo Sokomatola Jijini hapa na kuongozwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro.
Awali akifungua Mkutano huo Kandoro alisema lengo na madhumuni ya kikao hicho ni kujadili bajeti ya Mkoa kwa mwaka wa fedha 2012/2013 na Mwaka wa fedha 2013/ 2014 sambamba na kuangalia utekelezaji wake na changamoto zilizojitokeza katika ukamilishaji wa miradi kwa kila Halmashauri.
 Kandoro alisema Licha ya bajeti kuongezeka kutoka Shilingi bilioni 236 kwa mwaka wa fedha 2012/2013 hadi shilingi Bilioni 277.5 kwa mwaka wa fedha 2013/2014 bado changamoto kubwa ni ubora wa kazi zinazofanywa  na kusimamiwa na Halmashauri kutoridhisha kulingana na viwango vya fedha wanazotengewa.
Aliitaja changamoto nyingine kuwa ni hoja za mkaguzi wa hesabu za serikali kuendelea kujirudia kila mwaka hali inayoashiria Halmashauri kutokuwa makini na suala la matumizi sahihi ya fedha zinazotokana na kodi za wananchi kwa kuzitumia tofauti na malengo na muda unaokuwa umepangwa.
Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza kuwa utekelezaji wa miradi mwaka uliopita umeshindwa kufikia malengo kutokana na Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya kuendelea kuwa tegemezi katika bajeti zake kwa asilimia 95 ambapo Halmashauri zinaweza kujitegemea kwa asilimia tano pekee.
Alisema jambo la kutegemea ruzuku kutoka Serikalini siyo jambo la kufurahia hivyo kila Halmashauri ihakikishe inasimamia sheria ndogo zilizotungwa zinazohusu ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kuepuka kuwa wategemezi kwa kiwango kikubwa kama kilichopo kwa sasa ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mbeya.
                       
Mbali na hilo Kandoro aliagiza Viongozi wa Halmashauri kuwa karibu na wananchi kwa kuwashirikisha katika kazi za maendeleo ili kurudisha moyo wa uchangiaji na kupenda kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya Mkoa wa Mbeya na nchi kwa ujumla hali ambayo itasaidia kusukuma ukusanyaji wa mapato.
Aidha akisoma taarifa ya utekelezaji kwa mwaka uliopita Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja ambaye pia ni katibu wa kikao hicho alisema changamoto zilizojitokeza ni pamoja na kuchelewa kutolewa kwa fedha za maendeleo na wakati mwingine kutolewa kidogo kidogo hali hiyo mhusababisha kuchelewa kuanza kutekeleza kwa baadhi ya miradi husika.
Aliongeza kuwa kutokuwa na majengo bora ya ofisi na nyumba za viongozi kwa wilaya mpya kama vile Halmashauri ya Wilaya ya Momba na Busokelo zilizoanzishwa mapema mwaka huu na hivyo kutokuwa na miundombinu inayojitosheleza.
Alisema kuwepo kwa matumizi makubwa ya mafuta kwa ajili ya mapokezi na ziara za viongozi wa kitaifa , Wizara na washirika wa maendeleo wanapotembelea Mkoa na Wilaya na kuongezeka kwa gharama za usimamizi kutokana na kuongezeka kwa Halmashauri na Wilaya.
Mtunguja alisema changamoto nyingine ni uhaba wa vifaa muhimu vya ujenzi wa barabara katika Halmashauri na gharama kubwa za stahili za uhamisho na ajira mpya kwa watumishi wapya ndani ya taasisi za Serikali.

Na Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment