

Mh:Mwigulu Nchemba akiwasili eneo la Mkutano Kata ya Mkwiti Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara kwaajili ya Kufungua Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Udiwani,Licha ya Mvua Kubwa Kunyesha hadi mwisho wa Mkutano,Wananchi walikuwa radhi kunyeshewa lakini Wamsubiri Naibu Katibu Mkuu wa Chama Chao cha CCM ambaye kabla ya Kufika Mkutanoni alikuwa na Ziara ya Kufungua Matawi ya Chama,Kupokea Wananchama wapya waliojiunga na CCM Wilaya Ya Tandahimba na kutembelea Mashina ya Chama

Mh:Mwigulu Nchemba akitoa dakika Moja kwaajili ya Kumuombea Marehemu(aliyekuwa Diwani wa kata hii ya Mkwiti) ambayo hii loe inafanyiwa Uchaguzi Mdogo ilikuziba pengo lake Kiutendaji ndani ya chama na Serikali.


Huyu
alikuwa naye anawania Udiwani,Bahati mbaya kura zake hazikutosha wakati
wa Mchujo lakini ameamua kumuunga mkono MwanaCCM mwenzake,Na sasa Ndiye
meneja kampeni wa Mgombea wa CCM ndani ya Kata ya Mkwiti.


Naibu
Katibu Mkuu CCM Bara akimnadi Mgombea wa Udiwani kata ya Mkwiti wa
Chama Cha Mapinduzi Ndugu Nakatanda Arafa Twalib ambaye ni kada Mtiifu
wa Chama Cha Mapindizi kuanzia Ujana wake,
Licha
ya Mvua Kubwa iliyoanza Mapema tu kabla hata Mkutano kaunza,Wananchi
walijitokeza kwa wingi Kwenye Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za Udiwani
Kata ya Mkwiti,Uchaguzi mdogo huu unaofanyika takribani kata 27 Nchi
nzima kutokana na Madiwani waliochaguliwa Mwaka 2010 kwa sababu za Vifo
na Kujuzulu nafasi hizo zimekuwa wazi kwa Muda mrefu na sasa Tume
imeamua Uchaguzi Ufanyike tena.
Mh:Mwigulu
Nchemba akizungumza na Wananchi wa Mkwiti amewatolea Mfano mmoja
Mwepesi sana "Ukiwa na Touchi yako unahitaji mwanga,Betri ya Kwanza
Umeweka Vizuri(CCM-Rais),Betri ya Pili Umeweka Vizuri (CCM-Mbunge),Betri
ya Mwisho unaweka Gunzi(Upinzani) Itawaka?,HIvyo basi ni Muda Muafaka
Kwa WanaMkwiti Kuendelea kukiunga chama cha Mapinduzi kiendelea kuongoza
ndani ya Kata yao ili maendeleo yatokanayo na Ilani ya CCM yafanyike
kwa Ufanisi.
Kata
ya Mkwiti imekuwa Ikiongozwa na CCM tangu kuanzishwa Kwake,Na
kiamendeleo imepiga hatua Kubwa sana Baada ya Kuwekewa barabara ya Rami
inayowafanya wanuafaike na Shughuli za Kiuchumi ikiwamo Uuzaji wa Zao la
Korosho.
No comments:
Post a Comment