Saturday 18 January 2014

PICHA:MWIGULU NCHEMBA AVUNA WANACHAMA WAPYA 146,AIPASUA CUF WILAYA YA TANDAHIMBA

 Naibu Katibu Mkuu akizindua Shina la Wakereketwa Kata ya Chitama wilaya ya Tandahimba hii leo Tar.18/01/2014,Hapa akipandisha Bendera ya Chama iendelee Kupepea kama na Kuwaangaza wote wanaoamini katika Umoja na Amani ya Nchi yetu
 
Tawi limeshafunguliwa na Naibu katibu Mkuu Mh:Mwigulu Nchemba
Huyu alikuwa ni Katibu Mwenezi wa CUF kata ya Chitama,Ameamua kauchana na CUF na kujiunga na CCM,Hapa akivalishwa shati na Kofia kama Ishara ya Kukaribishwa Nyumbani,Kijana huyu amewasihi Vijana wenzake kuwa Kuwa Upinzani ni kupoteza muda tu kwani Vyama vya Upinzani ni Maslahi Binafsi.
Naibu Katibu Mkuu akitoa neno la Shukrani kwenye Mkutano wa ndani kwa Wanachama wapya waliojiunga CCM wapatao 146 katika kata Moja ya Chitama,WanaCCM wapya hao wamekula kiapo cha Utii kwa Chama na Nchi yao na wameahidi Kuipigania CCM iendelea kuongoza Nchi hii pia watakuwa Mabalozi kwa wenzao kujunga na Chama Cha Mapinduzi.
 
Wanachama wa CUF waliojisalimisha CCM kwaajili ya Kujiunga na Chama Cha Mapinduzi na Kuachana na CUF,Wao wanadai Wameitumikia CUF lakini hawajawahi Ona jambo lolote kutoka CUF la Maendeleo,Hivyo wameamua kurudi CCM chama cha Watanzania wote. 
Mh Mwigulu Nchemba akimpatia kadi ya uanachama mmoja wa Wanachama wapya wa CCM kata ya Chitama,Wilaya ya Tandahimba
Mh Mwigulu Nchemba alilazimika Kupiga Picha kwa Makundi na Wananchama Wapya,Hili hapa ni Kundi moja wapo la Wananchama wapya waliojiunga na Chama cha Mapinduzi kwa hiari yao.
Sehemu ya Wanachama Wapya wa CCM wakila Kiapo cha Utii kwa chama cha Mapinduzi na Nchi yao Tanzania.
 Kundi la Vijana waliojiunga na Umoja wa Vijana UVCCM pamoja na Chama cha Mapinduzi wakiwa katika Picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Mh:Mwigulu lameck Nchemba
 
Kundi lingine la Wanachama wapya wa CCM wakiwa kwenye Picha ya Kumbukumbu na Naibu Katibu Mkuu CCM Bara MWigulu Nchemba
 
Kundi Lingine la Wanachama wapya wakiwa na Naibu Katibu Mkuu na Viongozi wa Chama wilaya katika Picha ya Pamoja
Naibu Katibu Mkuu CCM Bara alipotembelea Shina la Chama cha Mapinduzi namba 15 Tawi la Tandahimba lenye Wanachama 28.Pia lipokea Wanachama 10 wapya ndani ya Shina hili.
Mmoja wa Wanachama wapya Shina namnba 15 akipokea Kadi ya Uanachama wa Chama Cha Mapinduzi kutoka kwa Mh:Mwigulu Nchemba.

Hili ni Shina lingine la Wakereketwa Tandahimba Mjini lililofunguliwa na Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba,Vijana waliofungua Tawi hili wamejiweka pamoja kwaajili ya Kufanya kazi mbalimbali za Maendeleo,Wao ni Vijana watiifu kwa Chama cha Mapinduzi na Nchi Yao na nimabalozi wa Amani na Mshikamano kupitia CCM.

4 comments:

  1. kiogozi wangu sasa nyota yako imeanza kungara zaidi, maona yangu juu yako yanazidi kuongezeka, kaka ongera sana mungu wangu akulinde katika utendaji wa kazi yako, hofu ya mungu ndani yako iweku kuu maana nafsi hiyo ni kubwa sana inaitaji uwepo wa mungu karibu yako. nampongeza mama watoto wako kwa sala zake daima uwapo safari au bungeni au katika shughuli zako za chama, ndugu kiongozi wangu tupo pamoja sana katika harakati za kujienga na kukiongezea chama heshima kwa wananchi wa tanzania, hekima na busara zimejaa ndani yako tunategemea utumishi uliotukuka, mungu ibariki tanzania, ibari ccm na mbariki comred Mwigulu AMEN.

    ReplyDelete
  2. Hongera sana mh., hakika umestahili, Mungu akuongoze pia akupe hekima kama mfalme Suleiman.
    Siku unaapishwa, naomba niwepo nikuvike taji la ushindi.

    ReplyDelete