Naibu
Katibu Mkuu CCM Bara Mh;Mwigulu Nchemba hii leo ameingia Mkoa wa Iringa
kwaajili ya Kufanya Kampeni za Uchaguzi mdogo wa Udiwani unaoendelea
Nchini.Picha ni Mh;Mwigulu Nchemba akihutubia mamia ya Wananchi
waliojitokeza kwenye Uwanja wa CCM kitongoji cha Mawambala Kata ya
Ukumbi Wilayani Kilolo mapema hii leo tar.29.01.2014.Ki historia Kata ya
Ukumbi haijawahi kutawaliwa na Upinzani,na Jimbo la Kilolo linaongozwa
na CCM kwa nyanja zote za Udiwani,na serikali za Mitaa zote.
Mh;Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye Mkutano wa hadhara viwanja vya CCM kata ya Ukumbi.
Naibu
Katibu Mkuu akimnadi Mgombea wa Udiwani kwa Chama Cha Mapinduzi Ndugu
Gift Emmanuel hii leo Kata ya Ukumbi wakati wa Mkutano wa hadhara wa
kunadi sera za Chama Cha Mapinduzi kwa Wananchi.
Naibu
Katibu Mkuu CCM Mh;Mwigulu Nchemba ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Fedha(sera) akisisitiza Kuwa CCM imeiongoza Kata ya Ukumbi tangu miaka
37 iliyopita,Kunamaandeleo mengi yamefanyika ikiwamo Ujenzi wa
Barabara,Zahanati,Mashule na Pembejeo za Kilimo,Na kwakuwa Diwani
aliyefariki alikuwa wa Chama Cha Mapinduzi,hivyo Wanaukumbi wahakikishe
wanampata Diwani mwingine wa CCM iliaendeleze utekelezaji wa Ilani ya
CCM kwenye kata hiyo.Ni rahisi sana kutimiza ilani yote kwa Wanaukumbi
endapo mtamchagua Diwani wa CCM kwa sababu CCM ndio Chama kinachounda
Dola pia ndicho Chama kinachotekeleza ilani kwa sasa,Kuchagua Upinzani
ni sawa na kujizibia maendeleo kwa sababu Upinzani hawana Ilani yoyote
ya Kutekeleza kwa Kata yenu,Vilevile huu sio Uchaguzi Mkuu kwamba Diwani
atabadilisha Serikali,Serikali iliyopo madarakani niya CCM na Shughuli
zote za maendeleo zinasimamiwa na CCM,Hao wengine ni wapinzani wa kila
kitu na mkiwakaribisha hapa watakuja kuwaletea Vurugu mpoteze amani
mliokuwa nayo Tangu uhuru.
Mh;Mwigulu
Nchemba akiagana na Wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye Mkutano wa
hadhara wa Chama Cha mapinduzi kitongoji cha Mawambala,Kata ya Ukumbi
Mkoani Iringa.Amewaomba Tar.09.02.2014 Wanachi wote kujitokeza Kupiga
kura kwa wingi kuichagua CCM iendelee kuongoza kata ya Ikumbi chini ya
Diwani Gift Emmanuel.
Picha zote na Habari Kwanza Blog
No comments:
Post a Comment