Naibu
Katibu Mkuu CCM Bara Mh;Mwigulu Nchemba akiwasili kwenye Uwanja wa
Mkutano Kata ya Kibindu Wilaya ya Bagamoyo, Mkoani Pwani hii leo Jioni
kwaajili ya Ufunguzi wa kampeni za Uchaguzi wa Udiwani CCM kwenye kata
hiyo hii leo tar.27.01.2014.Mh;Mwigulu
Nchemba akimpatia Kadi ya Uanachama wa CCM mmoja ya Wananchi walioamua
kujiunga na Chama Cha Mapinduzi kwa hiari yao hii leo ndani ya kata ya
Kibindu Wilayani Bagamoyo.
Sehemu
ya Kundi Moja la Wananchi waliojiunga na Chama Cha Mapinduzi wakila
Kiapo cha Utii kwa Mujibu wa katiba ya CCM.Hii leo Mh;Mwigulu Nchemba
amekabidhi kadi kwa Wanachama wapya 66 kwenye kata ya Kibindu.
Akiwa
njiani Kuelekea Uwanja wa Mkutano,Vijana wakereketwa wa Chama Cha
Mapinduzi Kitongozi cha Kwamasanja walimuomba Naibu Katibu Mkuu
awafungulie Shina lao kwaajili ya Kuimarisha Umoja wa Vijana na shughuli
za Kiuchumi zinazofanyika mtaani hapo na WanaCCM.
Mjumbe
wa Mkutano Mkuu wa Siasa Mkoa wa Pwani kwa Chama Cha Mapinduzi
Ndugu.Imani Madega akiwasalimia Wananchi waliofurika viwanja vya soko
kata ya Kibindu.Madega amewaomba Wanakibindu kufanya maamuzi sahihi
katika Maisha yao kwa kumchagua Mgombea wa CCM kwa sababu ndiye mwenye
Ilani inayotekelezwa kwenye kata hiyo.
Mbunge
wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Fedha Mh;Adam Malima akisalimiana na
Wananchi waliofika kwenye Ufunguzi wa Kampeni za Udiwani kata ya Kibindu
hii leo.
Mh;Mwigulu
Nchemba akiwasalimia Wananchi mara baada ya Kupandwa Jukwaani kwaajili
ya kuanza kuhutubia Ufunguzi wa Kampeni za Udiwani kata ya Kibindu.
Huu
ni Upande wa Mashariki wa Jukwaa,Mamia ya Wananchi wakimsikiliza
Mh;Mwigulu Nchemba ambaye sehemu Kubwa ya Hotuba yake amewaomba sana
WanaKibindu kufanya kampeni kwa Amani na Utulivu,Kupuuzia Wote wanaodai
Miaka 50 CCM haijafanya kitu ndani ya Jimbo la Bagamoyo ili hali
Barabara, Maji,Umeme(sola),Shule na Vituo Vya Afya vimejengwa ndani ya
Kata ya Kibindu kwa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Upande
wa Kaskazini wa Jukwaa,Mh:Mwigulu Nchemba akiwasisitizia jambo wananchi
kuhusu CHADEMA na namna wanavyosababisha mauaji kwenye Mikutano ya
hadhara ili tu wapate mtaji wa kisiasa.Mwigulu amesema Watanzania
wajiulize kuna vyama vya siasa 21 vyenye usajili wa Kudumu ndani ya Nchi
yetu,Lakini kwa muda wa Miaka 3 tu CHADEMA wameshasababisha Vifo zaidi
ya 10 kwenye Mikutano yao,Wakati Vyama Vingine vyote hata mkwaruzano tu
haujawahi kutokea kwenye mikutano yao.
CCM"Tumesimamisha
mgombea Kijana,anakubalika na Wakazi wote wa Kibindu,Mchagueni Ndugu
Mkufya Ramadhani kuwa Diwani wenu hapa aendeleze yale yalioachwa na
Marehemu Rajabu Almas aliyekuwa Diwani(CCM) wenu hapa.Msijaribu kugeuza
Kibindu eneo la majaribio kwa Wapinzani,wameshindwa kujiongoza wao ndani
ya chama chao,Wameshindwa kuongoza Halmashauri mbalimbali walizopewa
waongoze(Mwanza n.k),Hivyo hawana sifa za kuongoza Jamii yenye kiu ya
maendeleo kama hii ya Kibindu,watawapotezea muda na Ipo siki wataleta
Maandamano huku ilihali mmekuwa mkiishi kwa Amani na Upendo."
Mh;Mwigulu
Nchemba akimnadi Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Mkufya Ramadhani
kwa Wakazi wa Kibindu waliojitokeza kwa wingi sana kwneye Mkutano huu wa
Ufunguzi wa kampeni.'
Mkutano
Umeshamalizika,Mh;Mwigulu Nchemba anaagana na Wananchi waliojitokeza
kwenye Mkutano huu wa Ufunguzi wa Kampeni za Uchaguzi mdogo wa Udiwani
unaoendelea Kata ya Kibindu,Wilaya ya Bagamoyo.
Picha zote na Habari Kwanza Blog
No comments:
Post a Comment