Naibu katibu Mkuu wa
CCM Bara Mh;Mwigulu Nchemba hii leo 27/01/2014 asubuhi amewasili Mkoa
wa Tanga akitokea Arusha kwenye Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi mdogo wa
Udiwani kata ya Sombetini.Mh;Mwigulu Nchemba amekuwa kwenye ziara ya
Kichama ya Kuzindua kampeni za Uchaguzi wa Udiwani kata mbalimbali
Nchini,Akiwa ameanzia Mkoa wa Mtwara(Tandahimba),Mkoa wa
Manyara(kiteto),Mkoa wa Arusha(Sombetini) na hii leo ameingia Mkao wa
Tanga na Jioni ya Leo atakuwa Bagamoyo kwenye Uzinduzi wa Kampeni za
Udiwani Kata Kibindu.
Naibu
Katibu Mkuu licha ya kuendesha Ufunguzi wa Kampeni za Uchaguzi wa
udiwani,Pia amekuwa akifanya Vikao vya ndani vya Mkoa husika anaofika
kuzindua Kampeni.Vikao vya ndani vya Watumishi wa Chama Cha Mapinduzi
vimewa vikihusisha Makatibu wa Mikoa na Wilaya na Jumuia zake
zote.Ameshafanya Vikao hivyo Mkoa wa Mtwara,Manyara,Arusha,Hai,Moshi na hii
leo ameshatua Tanga kwaajili ya Kikao hicho cha Watendaji wa Chama Mkoa
wa Tanga.
Picha
hapa chini ni Kikao Kianchoendelea Muda huu Tanga cha Watumishi wa
ndani wa Chama kabla ya Kuondoka kuelekea Mkoa wa Pwani.




Picha zote na Habari Kwanza Blog
No comments:
Post a Comment