Monday, 24 February 2014

TASWIRA WATANZANIA NCHINI MAREKANI(DMV) WALIVYOADHIMISHA MIAKA 37 YA KUZALIWA KWA CHAMA CHAO CCM

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiingia ukumbini siku ya Jumapili Feb. 23, 2014 kwenye sherehe ya maadhimisho ya miaka 37 ya CCM yaliyofanyika College Park, Maryland na kuhudhuriwa na wafuasi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi DMV.


Meza kuu kutoka kushoto ni Ismail (katibu wa Vijina CCM DMV) George Sebo (mwanyekiti CCM DMV) Mhe. Liberata Mulamula (Balozi wa Tanzania nchini Marekani), Mama Kimolo (kitengo cha UWT) na Phanuel Ligate (CCM tawi la California)


Balozi Liberata Mulamula akiwa meza kuu na mwenyekiti wa CCM DMV George Sebo

Balozi Liberata Mulamula akiongea na wanaCCM DMV na kutoa historia ya chama hicho na kuongelea maswala ya mchakato wa rasimu ya katiba kuhusu swala la raia pacha ukiwemo umuhimu wa bima ya WESTADI kwa ajili ya kusaidia misiba inapotokea na kuwakumbusha Watanzania Nchini Marekani kuhusu sherehe ya miaka 50 ya muungano inayotarajiwa kufanyika Kitaifa Washington, DC April 26, 2014 na kuelezea siku hii ndio siku pekee inayotambulika nchini Marekani.


Mwenyekiti CCM DMV akiongea machache na baadae kumkaribisha Balozi Liberata Mulamula.


Balozi Liberata Mulamula akisaidiwa na Mwenyekiti CCM DMV kukata keki



Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa CCM DMV.


Balozi Liberata Mulamula akifungua dansi na wanachama wa CCM DMV akiwemo mwenyekiti George Sebo.

Kuona picha zaidi bofya hapa

No comments:

Post a Comment