Mh:Mwigulu Nchemba akisalimiana na aliyekuwa Mbunge wa Iramba Mwaka 2005-2010 ambaye kwa sasa ni MNEC-CCM wa Iramba.
Mh.Mwigulu
Nchemba,Naibu waziri wa Fedha kiwa Meza Kuu tayari kwenye Eneo la
Mkutano Viwanja vya Stand ya Kiomboi Jimboni Kwake Iramba,
Naibu
Katibu Mkuu CCM-Bara Mh;Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi wa
Iramba waliofika Viwanja Vya Stendi ya Kiomboi kwaajili ya Mkutano wa
Hadhara wa Mwigulu wa kuzungumza na Wananchi kuhusu Miradi ya Maendeleo
Mbalimbali pia Kusikiliza Kero zinazowakumba Wananchi wake ndani ya
Jimbo la Iramba.
Sehemu ya Mamia ya Wananchi waliofika Kwneye Mkutano Wa hadhara wa Mh;Mwigulu Nchemba hapa Kiomboi hii leo 20/02/2014.
Mh;Mwigulu Nchemba Mbunge wa Iramba akizungumza na Wananchi wake hii Leo Viwanja vya Stendi Kiomboi.
Na.Mwandishi Wetu.
Mbunge
wa Iramba Mh;Mwigulu Lameck Nchemba,Naibu Waziri wa Fedha na Naibu
Katibu Mkuu CCM-Bara hii leo 20/02/2014 amefanya Mkutano wa hadhara
Makao Makuu ya Wilaya ya Iramba,Viwanja Vya stendi ya Kiomboi kuzungumza
na Wananchi wake kuhusu Miradi ya Maendeleo ndani ya Jimbo lake na Kero
kutoka kwa Wananchi.
Akizungumza
na Wananchi wa Iramba,Mh:Mwigulu Nchemba amesisitiza kuhusu Matumizi na
Utunzani Mzuri wa Fedha za Umma"NImekuja hapa kutoa mrejesho wa
shughuli mbalimbali za Maendeleo zinazofanyika ndani ya Kata zetu/Jimbo
letu,Lakini Kubwa lililonileta ni kuhusu Mahesabu na Utunzaji wa Fedha
za Umma.Kumekuwa na tabia ya Watumishi wa Serikali kukalia Kusoma Mapato
na Matumizi kwa Wananchi wao,Hili ni Jambo lisilokubalika Kabisa
Kabisa,Viongozi wa serikali wanaojua Wajibu Wao ni Lazima waweke wazi
Mapato na Matumizi kwa Wananchi wao."Amesema Mwigulu.
Mh:Naibu
Waziri akaongeza kwa kusema"Naagiza kwa Mkuu wa Wilaya,Hili ni agizo na
sio Ombi,Naomba awachukulie hatua kali sana Viongozi wote waliokalia
Kusoma Mapato na Matumizi kwa Wananchi wao,hakikisha unafuatilia fedha
za miradi zote zilizopelekwa kwenye kila kata.Mimi Kama Mbunge wenu hadi
sasa kila kata ya Jimbo hili nimeshapeleka zaidi ya Miloni 3 kwa kila
kata kwaajili ya Kusaidia Shughuli za Maendeleo.Naagiza Mkuu wa WIlaya
kufauatilia fedha hizo,pamoja na fedha zingine za Maendeleo kuhakikisha
zimefanya kazi iliyokusudiwa.Kwa yeyote mwenye taarifa kuhusu Kiongozi
wa serikali kutumia vibaya Fedha za Umma naomba atoe taarifa kwa Mkuu wa
WIlaya au Ofisi yangu ili Sheria stahiki zichukuliwe."
Mbali na hapo Mh;Mwigulu Nchemba ametoa Ambulanche Moja kwaajili ya Wananchi wa Kata ya Shelui,Pia ametengeneza Ambulance ya Kata ya Ndago na imeshapelekwa Hospital ya Ndago kwaajili ya kusaidia Wagonjwa.Mbali na huduma hiyo ya Kiafya,Mh:Mwigulu Nchemba ameshaorodhesha Vijiji mbalimbali vya kata zote kwenye Mpango wa Kupitisha Umme,Kuna Vijiji kata ya Ndago vimeshawashwa Umme.Kazi ya Kuweka Nguzo za Umme kwenye Vijiji vilivyopo kwenye mpango wa Umme mwaka 2014/2015 imeshaanza.
Pia
Mh:Mwigulu Nchemba ametumia Mkutano huu kuwaeleza Wananchi kuwa,Ameamua
kulivalia Njuga swala la Sera ya Manunuzi Serikalini.Sera ya Manunuzi
imekuwa ikiipa Serikali Mzigo mzito sana,Kwani Wazabuni wengi wamekuwa
wakitumia Mwanya huo kujipatia Fedha Nyingi tofauti na uhalisia wa
huduma inayotoelewa.Mh;Mwigulu Nchemba ametolea mfano kuwa,Duka lile
lile mtu wa kawaida ananunua Soksi kwa TSh.1000,lakini Duka lile lile
Kupitia Mzabuni wa Serikali Soksi Zile zile zinanunuliwa kwa Tsh. 7000.Hivyo
Serikali inapoteza Fedha nyingi sana kwenye Manunuzi ambayo Sheria yake
haijawa na Faida kwa Serikali zaidi ya kuwa mzigo.
No comments:
Post a Comment