Sunday, 30 March 2014

TASWIRA,MH:MWIGULU NCHEMBA ACHANGIA UJENZI WA KITUO CHA WATOTO YATIMA RUKWA KWA NJIA YA UIMBAJI,AZINDUA ALBAMU YA NYIMBO ZA INJILI YA BI;REHEMA.

Naibu Waziri wa Fedha(Uchumi) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Mh:Mwigulu Nchemba akikata Utepe na Kuzindua rasmi Albamu ya Nyimbo za Injili Zilizoimbwa na Bi.Rehema.Tukio hili limefanyika Victory Church Mabibo External hii leo Tar.30/03/2014.Bi.Rehema amezindua Albamu yake ya pili.Mwaka 2012/12 aliachia Albamu ya Kwanza iliyozinduliwa na Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda huko Rukwa.
 Bi.Rehema akishukuru Kwa Mgeni Rasmi kwa tendo la Kuzindua Albamu yake Rasmi aliyoielekeza kwenye Ujenzi wa Kituo Cha Watoto Yatima Wilayani Rukwa.Bi.Rehema akiingia kuzindua Albamu yake ya Pili Tangu aanze Kuimba nyimbo za Injili.
Kada wa Chama Cha NCCR akichangia Fedha kwenye Uzinduzi wa Albamu ya Bi.Rehema.
 Naibu Waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza na Washarika waliofika kwenye Uzinduzi wa Albamu ya Bi.Rehema.Mchekeshaji Kutoka EATV Comedy akiimba Wimbo wake wa Kumsifu yesu,Kwa sasa Msanii huyu anafanya Kazi ya Kutangaza Injili Kupitia Nyimbo za Kumtukuza na Kumsifu Yesu.
Mh:Mwigulu Nchemba akicheza kwa Kusifu Utukufu wa Mungu kwa Pumzi tunayoendelea Kutumia.Ni Kwa Neema tu.
 Mke wa Mh:Mwigulu Nchemba akimpongeza Mme Wake Mara baada ya Kucheza pamoja na Vijana wa Bi.Rehema wakati wa Kumsifu Mungu.
Sehemu ya Washarika waliofika Kushuhudia Tendo Kuu la Uzinduzi wa Albamu ya Bi Rehema hii leo hapa External Mabibo.
Mh:Mwigulu Nchemba akisisitiza Washarika na Makanisa yote Kushikamana Kuombea Taifa katika Kipindi hiki cha Bunge Maalumu la Katiba,Mwigulu amesema hiki ni Kipindi Kigumu sana kwa Taifa letu,Katiba Inatungwa kipindi amacho Dunia imechafuka kuna mambo mengi yasiyo na tija kwa Taifa tunahitaji Kuungana kuyazuia.Hivyo lazima tukio la Utunzi wa Katiba liwe la wazi,Kufichaficha Mambo kwa Siri ni hatari sana,hakuna haja ya Kujificha wakati tuliopo Bungeni wote ni Wawakilishi wa Wananchi hivyo Wananchi Mnahaki ya Kupata kile tunachokisimamia Bungeni.
 N/Waziri wa Fedha(uchumi) Mh:Mwigulu Nchemba akikabidhi Mchango wake kwa Bi.Rehema mara baada ya Kuzindua Albamu ya Mtumishi wa mungu huyu.Fedha hizi zinakwenda Moja kwa Moja kwenye Ujenzi wa Kituo cha Watoto yatima huko Mkoani Rukwa.
Bi.Rehema akishangilia na Kuuonesha Umma Mchango wa Mh:Mwigulu Nchemba katika Ujenzi wa Kituo cha Watoto Yatima huko Rukwa kwa Njia ya Uimbaji.
 "Kwa hiki nilichokitoa,Naomba nikawapelekee Marafiki Zangu na Wabunge wa Mkoa wa Katavi hizi CD ili wachangie kwenye Ujenzi wa Kituo cha Watoto Yatima" Mh:Mwigulu.
Mwenye Nguo ya Juu Rangi ya Njano ni Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Ndugu.Beatrice Mwaipaja akijumuika Kwenye Uzinduzi wa Albamu ya Bi.Rehema.
 Masanja wa EATV akiendelea Kuburudisha kwa Kumsifu Yesu kupitia Nyimbo zake.
Mwimbaji Daniel Thomas akiimba wimbo wake wa "IBADA NJEMA HUANZIA NYUMBANI" wakati wa Uzinduzi wa Albamu ya Bi.Rehema.
 Mh:Mwigulu Nchemba alivutiwa na Uimbaji wa Kijana huyu Daniel Thomas na Kuamua Kumvisha Skafu yake ya Bendera ya Nchi yetu.Lilikuwa ni tukio la Kuvutia lililovutia Wengi sana na Kuamsha nderemo na Vifijo kwenye Uzinduzi wa Albamu hiyo.Meza Kuu wakiendelea Kumsifu Bwana kwa kushirikiana na Waimbaji mbalimbali waliokuwa wakipanda Jukwaani Kusifu.
Bi.Magadalena Nyambalya akiimba wimbo wake wa "SAFARI YA MBINGUNI" Wakati wa Uzinduzi wa Albamu hiyo ya Bi.Rehema.
 Mke wa Mh:Mwigulu Nchemba akisalimiana na Mwimbaji Maarufu Nchini Ndugu Upendo Nkone mara baada ya Kupanda Jukwaani kwaajili ya Kumsifu Mungu.
Mwimbaji Upendo Nkone aliomba Kuimba pamoja na Mh:Mwigulu Nchemba na Mke wake wimbo wa mmoja kwaajili ya Kumtukuza Mungu. Wimbo uliombwa ni "USIFURAHI JUU YANGU".
 Wimbo wa Niacheni Nimbe,Mungu amejibu Maombi Yangu ndio Unaendelea hapa,Ni Wimbo wa Upendo Nkone ambao Ukiimbwa popote ni Lazima  Utambue Uwepo wa Mungu.
Mwimbaji na Mchekeshaji Msanja Mkandamizaji akisifu wakati wa Uzinduzi wa Albamu ya Bi Rehema hii leo Victory Church Ubungo-External.
 Mh:Mwigulu Nchemba akimtunza Mwimbaji Masanja Mkandamizaji.
Musa Baba wa Imani akiwatoa wana wa Israel Nchi ya Misri na kuwapeleka Nchi ya Ahadi.
 Hatimaye Shughuli Nzima imemalizika Salama na Kwa Maombi Makubwa ili kituo kile cha Watoto Yatima kikapate Kusimama na Kutumika Sawasawa na Mapenzi ya Bwana.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mh:Mwigulu Nchemba hii leo ameshiriki ibada ya Uzinduzi wa Albamu ya Nyimbo za Injili za Mwimbaji Rehema kutoka Rukwa iliyofanyika Victory Church Ubungo-External.Mbali na Ufunguzi huo Mh:Mwigulu Nchemba amechangia Zaidi ya Milioni 10 Kwaajili ya Ujenzi wa Kituo Cha Watoto Yatima huko Rukwa kitakacho Simamiwa na Mwimbaji Rehema.Mh:Mwigulu Nchemba ameomba Watanzania kushikamana na kuasaidiana katika Shida,Kujali na Kuwatunza Watoto Yatima.
Pia Mwigulu NChemba ametumia nafasi hiyo Kuwasihi Washarika,Wachungaji na Maaskofu Kuendelea Kuliombea Taifa hili kipindi hiki cha BUnge la Katiba.Amewasihi Wananchi waache Kuangalia Vyama vya Siasa,Waangalie hoja na sio nani Katoa hoja.Watu Wanataka Kutumia Mwanya wa Uundaji wa Katiba Mpya kupitisha Mambo yatakayo ligawa Taifa sikuz a Usoni,Hivyo ni dhahiri Kila Mjumbe wa Bunge la Katiba ni lazima akubali Kuwa Muwazi kwa Watanzania waliomtuma Kushiriki kazi ya Kutunga Katiba Mpya,Kitendo cha Kufanya Mambo kwa Siri ni Kuwanyima Watanzania haki yao ya Kujua kile walichowatuma Wajumbe pale Dodoma.
Picha/Maelezo na Sanga Festo

No comments:

Post a Comment