- Zaidi ya watu 700 wajiunga na CCM akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Kata ya Rungwe mpya.
- Asema mtaji wa vyama vya Upinzani ni matatizo ya wananchi na hawasaidii katika kuyatatua badala yake wanataka wananchi waendelee kuumia ili wao wajijenge kisiasa .
Katibu Mkuu
wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha
Nyenge kata ya Kurugongo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ikiwa sehemu ya
ziara yake mkoani humo.
Mbunge wa
Viti Maalum Ndugu Josephine Gezabuke akihutubia wakazi wa kijiji cha
Nyenge kata ya Kurugongo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika
kijijini hapo na mgeni wa heshima alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu
wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya Tawi CCM
kata ya Kurugongo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
Katibu Mkuu
wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akila karanga za kuchemsha pamoja na
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye baada ya kumaliza mkutano
mkubwa wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya michezo shule ya Msingi
Nyenge kata ya Kurugongo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
Balozi Ali Abeid Karume akicheza ngoma ya asili ya Kasulu wakati wa mapokezi kwenye viwanja vya Stendi ya taxi Kasulu mjini.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akihutubia wakazi wa
Kasulu mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kituo cha
stendi ya Taxi na kuwaambia wananchi hao CCM imedhihirisha kuwa komavu
kwenye demokrasia ya kweli na hali inavyoendelea hivi sasa wapinzani
wameanza kupotea kabisa kwenye siasa kwani kwenye uchaguzi wa madiwani
kati ya kata 27 walipata tatu, ubunge Kalenga na Chalinze wameanguka
vibaya sana .
Katibu Mkuu
wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Kasulu mjini na
kuwaambia kuwa CCM itaendelea kuhakikisha maendeleo yaliopangwa yanazidi
kutekelezwa licha ya kuwa na changamoto mbali mbali hasa wapinzani
kutaka wananchi wateseke ili wao wajijenge kisiasa alisema sivyema vyama
pinzani kutafuta sifa kwenye matatizo ya wananchi.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwainua juu wanachama wapya waliojiunga
leo kutokea vyama vya upinzani kulia ni Ndugu Nahasoni Kigamba alikuwa
Mwenyekiti wa CUF kata ya Rungwe mpya na Adolf Yanda aliyekuwa Katibu wa
Chadema kwa wanafunzi wa chuo cha SUA,katika mikutano miwili mikubwa ya
leo zaidi ya wanachama 700 walijiunga na CCM .
C C M OYEEEEE
ReplyDelete