

Mh:Mwigulu
Nchemba akifurahia Jambo na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake-DMV wakati
akiwasili kwenye Uzinduzi wa Shina la CCM-Maryland.



Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi na MC wa Shughuli ya Ufunguzi wa Shina la CCM akiwajibika kuweka ratiba sawa Ukumbini,
Makada watiifu wa Chama cha Mapinduzi hapa Maryland.



Watanzania na Wana-CCM wakiwa tayari Kuitumikia Nchi yao na Chama chao.






Wana-CCM Wakipata Ukodak.









Mh:Mwigulu
Nchemba akifurahia jambo mara baada ya Mwanachama wa CCM kusema
kutokana na Mwenendo wa Siasa zake atakuwa kuwa Kiongozi Mkubwa katika
Nchi hii,na Wana-CCM wataendelea Kumuunga Mkono katika kazi zake.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake-DMV -CCM akitoa Ombi rasmi kuwa Mke wa Mh:Mwigulu Nchemba awe mlezi wa Jumuia ya Wanawake=DMV.



Mh:Mwigulu Nchemba akishiriki Chakula kilichoandaliwa kwenye hafla ya Ufunguzi wa Shina la CCM-Marland-Marekani.

Mwenyekiti wa Shina la CCM-Maryland Ndugu Mrisho Mzese akishiriki Chakula kilichoandaliwa kwenye Ufunguzi huo wa shina.
Furaha ya Kukutana na Kiongozi wa Kitaifa ni pamoja na Kuweka Kumbukumbu ya Picha kama hivi.
Mwenyekiti
wa Jumuia ya Wanawake-CCM hapa Marekani(Watatu kutoka Kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja na Baadhi ya Wanawake walifika kwenye hafla ya
Uzinduzi wa Shina la CCM-Maryland.



Viongozi
wa Chama wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu-CCM_Bara Mh:Mwigulu Nchemba
kupiga picha ya pamoja na Wanachama wapya wa Chama cha mapinduzi.Hii leo
Mh:Mwigulu Nchemba amepokea Wanachama 8 wapya waliojinga na CCM.
Kutoka Washington-DC.
Naibu
katibu Mkuu CCM-Bara Mh:Mwigulu Nchemba hii leo tar 27/04/2014
amezindua Shina la Chama cha Mapinduzi hapa Maryland tayari kwa kuanza
kuitumikia CCM na Wanachama wake.Ufunguzi wa Shina hili ni mwendelezo wa
kuhakikisha Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wanakuwa katika Mfumo
mmoja wa Kichama.
Akizungumza
na Watanzanai waliofika kwenye Uzinduzi huo,Mh:Mwigulu Nchemba
amesisitiza kwa Wana-CCM wanatakiwa kujenga mazingira ya Kuwa pamoja
mara kwa Mara kwaajili ya Kujenga Umoja na Mshikamano hasa Ukizingatia
wapo Mbali na Nyumbani Tanzania.
"Umoja
wenu ndio Ngao yenu kwa hapa Marekani,Naomba sana Mshiriki kwenye
Jumuia zenu na mshiriki kwenye Shughuli za pamoja zikiwamo hizi za
Kisiasa,Haitakuwa afya Kufunga Mashina na Matawi ya CCM Kwaajili ya
Kuvunja Umoja wetu,Tutumie Mashina haya Kutuimarisha zaidi"alisema
Nchemba.
Mbali
na hilo na Kudumisha Umoja,Mh:Nchemba ameendelea kusisitiza kuwa
Mchakato wa Katiba Mpya ni jambo Zuri sana lakini Kukosekana kwa Utashi
wa Kisiasa kwa Viongozi wa Kisiasa kunapeleka katiba ama kutopatikana au
Kuchelewa kupatikana.Hivyo ameomba Watanzania waliopo Marekani na Nchi
nyingine kaucha kushabikia Mambo yasiyokuwa na tija kwa Taifa lao ambayo
yatapelekea Utengano.
Zaidi
ameahidi Viongozi wa CCM Wataandaliwa Semina kwaajili kupata Mafunzo ya
Kuwa Kiongozi Mwadilifu na Mzalendo kwa Chama na Taifa letu.
Picha/Maelezo na Sanga-Festo /Washington DC
No comments:
Post a Comment