Thursday, 1 May 2014

VIDEO:MTANZANIA HUYU ASHINDWA KUJIZUIA NCHINI MAREKANI"MWIGULU NI RISING STAR,KIONGOZI MKUBWA WA TAIFA AJAYE"

Mtanzania Ndugu Bruno aliyekaa Upande wa Kuliya ndiye aliyeshindwa kujizuia na Kuamua kuaniaka hisia zake kuwa Mh:Mwigulu Nchemba ni "RISINGI STAR"
Ni nadra sana mtu Kusimama mbele ya Umma na Kuonesha hisia Zake kuhusu Kiongozi Flani namna anavyomkubali Kiutendaji na kufikia hatua ya Kusema anatamani Kuona Siku moja Nchi yake Inaongozwa na Kiongozi huyo.Lakini imetokea kwa Mtanzania huyu(Pichani) aliyeamua kunika hisia Zake kwa Watanzania waliokusanyika pamoja kwenye Ufunguzi wa Shina la CCM-Maryland Nchini Marekani namna anavyopendezwa na Utendaji kazi wa Mh:Mwigulu Nchemba,na kudiriki Kusema "Watamdharau,Watamdhihaki,Lakini ipo siku Watamkubali na  Atawaongoza" akatolea Mfano kuhusu Rais wa Marekani Barack Obama alivyodhihakiwa hapo awali wakatia anajiandaa Kugombea Urais awamu ya Kwanza na yapili,lakini hii leo Obama ni nani kwa Marekani?
Hivyo anasisitiza Kunahaja kwa Watanzania Kumuunga Mkono Mwigulu Nchemba katika siasa Zake kwa sababu zimejikita kutetea Watanzania,Kuimarisha Uzalendo na Kupigania Umoja na Mshikamano ndani ya Taifa letu.Angalia Video hii hapa Chini ya Mtanzania huyu (Bruno)akitoa hisia zake kwa Mh:Mwigulu nchemba.
Hii hapa Chini ndio Video iliyomgusa sana Mtanzania huyu hadi Kufikia hatua ya Kusema Mh:Mwigulu Nchemba ni Rising Star na Kiongozi Mkubwa ambaye anategemewa Kuja Kutokea katika taifa hili la Tanzania.
Angalia Vidoe hii hapa.

1 comment:

  1. ndugu mwigulu nchemba mungu akubaliki kwa kutetea wanyonge . hongera ccm,

    ReplyDelete