Mh:Mwigulu
Nchemba akiwasili Viwanja vya Fire Mjini Morogoro kwaajili ya Mkutano
wa Hadhara wa Kuzungumza na Wakazi wa Mwananchi.Mh:Mwigulu akipata mapokezi na wakazi wa Morogoro Mjini.
Mh:Mwigulu Nchemba akifurahia jambo na Mbunge wa Morogoro Vijijini kwenye Mkutano huo.
Vijana wa chama cha
Mapinduzi wakitoa buruduani ya Nyimbo.Kulia ni Mwenyekiti wa Vijana Wilaya ya Morogoro Mjini akiwasalimia Wananchi.Kulia
ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Mzumbe akizungumza
kuhusu Ubora wa Serikali mbili na namna yeye na Wasomi wengine Nchini
wamepanga kuhakikisha Serikali mbili zinapita kwenye katiba Mpya
itakapofika hatua ya Kura ya Wananchi.Katibu
wa Mkoa wa Vyovikuu Nchini Ndugu Ndubi Hagai akishangiliwa na wanachama
wa Chama cha Mapinduzi kutoka Vyo vya Mzumbe,SUA n.kMh:Abood
akiwashukuru Wananchi wake kwa Kumuunga mkono kwenye Utekelezaji wa
Ilani ya chama cha Mapinduzi na amesisitiza Morogoro ni Ngome ya CCM na
kamwe haitakwenda Upinzani.Mbunge wa Morogoro Vijijini akisalimia Wananchi.Comrade
Mwigulu Nchemba akizungumza na Wakazi wa Morogoro Mjini,Kubwa
amesisitiza kuwa Huu ni wakati wa Kupigania Ajira kwa Vijana na sio Muda
wa Kurumbana kuhusu Idadi ya Serikali,Idadi ya Serikali hainatija kwa
Watanzania kwa sasa,Watanzania wanahiji Maendeleo tu.
CCM Oyeeeehhh!!!Sehemu ya Wananchi wa Morogoro wakishangilia Chama cha Mapinduzi.
Mkutano Unaendelea!!Mambo poaa!!!
Mh:Mwigulu
Nchemba akiwaaga wakazi wa Morogoro Mjini mara baada ya Kumalizika kwa
Mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Mamia ya Wakazi wa Morogoro Mjini.'
Huu
ni Mwenedelezo wa Mikutano ya Mh:Mwigulu Nchemba ya kuzungumza na
Watanzania kuhusu Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi,Mchakato
wa Katiba Mpya na Kujipanga kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na
Uchaguzi Mkuu mwaka 2015,Wiki iliyopita Mh:Mwigulu Nchemba pia
alizungumza na Wakazi wa Iringa Mjini viwanja vya Mwembetogwa kuhusiana
na mambo tajwa hapo juu.
Mwigulu
Nchemba ambaye ni Naibu Katibu Mkuu CCM_Bara ametumia sehemu Kubwa ya
Hotuba yake kwa Wakazi wa Morogoro kuwaelimisha kuhusu Mchakato wa
katiba Mpya ulipofikia na kile kinachozungumzwa na wanaojiita UKAWA
kwenye Mikutano yao,Nchemba akizungumza kwa Msisitizo wa hali ya Juu
amesema "UKAWA ni genge la Watu wachache waliodhamiria kusaka Madaraka
kupitia idadi ya serikali,Wanazunguka Nchi Nzima kudanganya na Kuwagawa
Watanzania kuhusu Serikali tatu,Haijawahi tokea wakatumia gharama kubwa
kutekeleza miradi ya Maendeleo au Kuwaelimisha Watanzania kuhusu
Kujiajiri,Wanatumia Fedha za Misaada na ruzuku kuzunguka Angani
kuwahadaa Watanzania kuwa serikali tatu ni Suruhisho la Matatizo,Naomba
kuuliza Serikali ya tatu Itajishughulisha na
Afya,Elimu,Umeme,Barabara,Maji? Sasa tutatengenezaji Serikali
inayokusanya kodi tu za Watanzania na kodi hiyo haitumiki kwenye mambo
muhimu kwa Watanzania kama Afya,Elimu n.k?
Pia
Watanzania Watambue wazi kuwa,Hakuna Serikali inayoendeshwa kwa gharama
ndogo,Serikali ya tatu ikija hapa kodi itapanda na Uwezekano ni Mkubwa
sehemu moja ya Muungano ikashindwa kuchangia Serikali hiyo ya tatu na
hatimaye tukaigwa Nchi kwa Misingi ya Utanganyika na Uzanzibari kitu
ambacho ni dhambi kubwa na haitatuacha salama.
Kuhusu
Uchaguzi Ujao wa serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu,Mh:Mwigulu Nchemba
amewaomba Watanzania kuwa na Imani na chama cha Mapinduzi na Wandelee
kuichagua CCM kama ilivyofanyika chaguzi za Nyuma na hata hizi za
Karibuni,Kata 23,Majimbo ya Kalenga na Chalinze.Mkataba wa CCM na
Watanzania ni Maendeleo na sio Kuzunguka na Helkopta kwa gharama kubwa
kuitukana Serikali an Viongozi wake.
Mwisho
Mh:Mwigulu Nchemba amesisitiza kuwa "Kitendo cha Wabunge wa Upinzani
kutoka Nje ya Bunge liwe la Katiba au la Jamhuri ni kudhihirisha wazi
kuwa hawafai hata kidogo kupewa Uongozi,huwezi kuwa na Kiongozi
anayesusa kuwatumikia Wananchi wake,Wanasusia bajeti ya Nishati na
Madini wanategemea Wananchiwao nani akawaombee Umeme
Bungeni?Inasikitisha kuona Kambi ya Upinzani yenye Viongozi wabovu kama
Tanzania,Viongozi wasiokuwa na VISION kuhusu Taifa lao,akili na mawazo
yao wameelekeza kwenye Ubinafsi na Upotoshaji kwa Watanzania.Wanasahau
kuwa Mwaka 2015 ni kesho kutwa na wengi wao ndio utakuwa Mwisho wao
kuingia Bungeni wajiandae kuwa Wageni wetu tu.
Picha/Maelezo na Sanga Jr.
No comments:
Post a Comment