Mh.Mwigulu
Nchemba akizungumza na Kondakta wa Gali lililopata ajali mara baada ya
Kumnasua kwenye roli hilo.Kijana anaonekana kuuguria maumivu makali
kwenye Mkono.Mh.Mwigulu
Nchemba akiangalia sehemu aliyokuwa amebanwa Kondakta wakati Roli hilo
likianguka na baadae kuinuka kutokana na kugonga Ukuta pembezoni mwa
Barabara ya Iringa-Morogoro.Mh:Mwigulu Nchemba akitoka huduma ya Kwanza kwa Majeruhi wa ajali hiyo.Huyu ni Dreva akijaribu kuwasha Gari hilo.Mh:Mwigulu Nchemba akiendelea kutoa huduma ya kwanza kwa Majeruhi kabla ya kumkimbiza kwenda hospitali ya WIlaya ya Mikumi.
Na.Festo Sanga.
Naibu
waziri wa Fedha na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mh:Mwigulu
Nchemba jana alifanya jambo kubwa na lakibinadamu kwa kuamua kusitisha
safari yake kwa muda akielekea Iringa iliasaidi Majeruhi wa ajali ya
Roli Kubwa lililokuwa likitokea Dsm kuelekea Barabara ya Iringa.
Ajali
hiyo ambayo ilitokea mbele ya Mh:Mwigulu Nchemba aliyekuwa nyuma ya
Roli hilo kabla ya Kugonga Ukuta na Kuanguka haikuleta madhara makubwa.
Mh:Mwigulu
Nchemba ambaye ni mara kadhaa amekuwa akisaidia kuokoa majeruhi kwenye
ajali anapokutana nazo barabarani,hata kwenye ajali hii alilazimika
kuhakikisha majeruhi wanaokolewa na kukimbizwa Hospitali kabla ya hatua
kubwa zaidi za Hospitali kuendelea,Katika ajali hiyo Mh:Mwigulu Nchemba
alitumia Boksi lake la Msalaba Mwekundu(First Aid Kit) kuhudumia
majeruhi hao iliwasitoke sana Damu.
Wananchi
na Madreva waliopata kusimama kwenye ajali hiyo,Walimpongea sana
Mh:Mwigulu Nchemba kwa namna alivyosaidia kuokoa Watanzania wenzake
kwenye ajali hiyo,Wengi walisikika wakiomba Viongozi wengine waige
mifano hii ya Mwigulu ya Kusimama na kuhudumia wahanga wa ajali,Kwa
sababu imekuwa ikitokea Viongozi wanapoona ajali hawasimami kwa madai
wanawahi ratiba za kazi zao.
No comments:
Post a Comment