Mh:Mwigulu
Nchemba akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr.Kone wakati
wakukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Maabara za Kisasa Katika Shule za
Jimbo la Iramba,Hapa ni Shule ya Kijiji cha Usule.Kufikia Tar.31/09/2014
Mkuu wa Mkoa anategemea Kumkabidhi Mh:Rais Jakaya Kikwete Maabara zote
za Shule za Sekondari zikiwa zimekamilika ndani ya Mkoa wa SIngida
kuendana na Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Mh:Mwigulu
Nchemba akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Usule waliofika
kusikiliza mambo mbalimbali ya Utekelezaji wa Shughuli za Maendeleo.Kwaya ya akina mama Kiji cha Usule wakitumbuiza mbele ya Mgeni Rasmi Mh:Mwigulu Nchemba(hayupo pichani).Vijana wakifurahia Ushindi wao katika Michuoano ya MWIGULU CUP,Hii ni timu ya Kijiji cha Usule.Akina mama wakionesha kadi zao za Chama cha Mapinduzi kuonesha kuwa wao bila CCM haiwezekani.Wananchi wakishangilia baada ya Kuona Nguzo za Umme zikipita kijijini kwao Ishara kuwa Umeme umewafikia.
Mh:Mwigulu akimsikiliza Mmoja wa Wazee wa kijiji cha Usule.Mkutano
unaendelea huku Mh:Mwigulu nchemba akiwafafanulia mambo mbalimbali ya
maendeleo wanakijiji wa Usule,Kubwa ni Usambazaji wa maji hapo Kijijini
ambao tayari umekwisha anza,Pia amesisitiza Kusuka nyaya za Umeme wakati
huu Umeme unapowekwa kwenye nguzo,Ukiingiza Umeme wakati huu mafundi
wakiwa wanasambaza nyaya ni Bei nafuu 27000/= tu.Ilikukamilisha
Ujenzi wa Maabara ya Shule ya Usule Mh:Mwigulu amechangia Mifuko 100 ya
Sementi na ameagiza kwenye Upungufu wowote Mwenyekiti wa kamati ya
Ujenzi atoe taarifa.Hivyo hivyo amesaidia Uchimbaji wa Bwawa la maji
kama Mpango wa Muda mfupi wakati Bomba za Maji zikiendelea Kusambazwa
kijiji chote cha Usule.Baadhi ya Vijaja Kijiji cha Kibaya wakiwa kwenye Jezi zao za MWIGULU CUP.Mh:Mwigulu
Nchemba akikabidhi Mchango wake wa bati 70 kwa Diwani wa kata ya
Mbelekesye kwaajili ya kuezeka Madarasa ya shule ya Mbelekesye
yaliyoongezwa.Pia amechangia Mifuko 100 na Mbao kwaajili ya kupau
madarasa hayo.
Wakati
hili likifanyika katika kijiji cha Kibaya,Mh:Mwigulu Nchemba jana
alikabidhi Mabati 320 kijiji cha Misuna kwaajili ya Ujenzi wa Zahanati.Wananchi wakibaya wakifurahia na Mbunge wao.
No comments:
Post a Comment