Hisia
za Wananchi wa Korogwe zikiwa zimeandikwa kwenye Bango hili kama
linavyosomeka,Hii imetokea Korogwe Mjini wakati Naibu katibu Mkuu CCM
Bara Mh:Mwigulu Nchemba alipofanya ziara ya kutembelea wilaya zote za
Mkoa wa Tanga hii leo.Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mh:Mwigulu Nchemba akisalimiana na
wananchi wa wilaya ya Pangani wakati wa ziara yake aliyoifanya kwa siku
moja(17.01.2014) kwa wilaya zote za Mkoa wa Tanga.Naibu
katibu Mkuu akiwasili Viwanja vya Tangamano-Tanga Mjini hii leo
kuzungumza na Wananchi wa Tanga,Kubwa amesisitiza wananchi kutijitokeza
kupiga kura,kufuatilia mapato na matumizi ya Halmashauri zao.Pia
amesisitiza kuwa Machinga wanaofanya kazi zao soko la Tangamano
wasichukuliwe kama sehemu ya Uchafu,bali serikali iwawekee Utaratibu
mzuri wa kufanya biashara zao.Wananchi wakigombania angalau kusalimiana na Naibu katibu Mkuu alipowasili Muheza Tanga hii leoNaibu katibu MKuu akisalimiana na Wananchi wa Kilindi hii leoMkutano ukiendelea wilaya ya Kilindi.Naibu
katibu Mkuu akizungumza na Wananchi wa Handeni hii leo wakati wa ziara
yake ya Kuhamasisha wananchi kuendelea kuiunga mkono CCM,Pia kujitokeza
kupiga kura.Wananchi wa Nkinga(Maramba) Mkoani Tanga wakisalimiana na Mh:Mwigulu NchembaComrade
Mwigulu Nchemba akiteta na Wananchi wa Handeni wakati alipofanya
mkutano wa kuzungumzia utekelezaji wa Ilani ya chama cha mapinduzi na
Umuhimu wa kujiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura.Hisia za Wananchi kwa Naibu katibu mkuu zikiwa zimeandikwa kwenye mabango wilayani Handeni.Sehemu ya mamia ya Wananchi wakisikiliza Mkutano wa Naibu katibu Mkuu wilayani Korogwe.Mh:Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi wa korogwe Mjini.Hisia za Wananchi wa Korogwe kwa Mwigulu Nchemba,hii inatokana na utendaji kazi wake unaogusa watanzania waliowengi.Mh:Mwigulu
Nchemba akizungumza na wananchi wa Korogwe Mjini kuhusu utekelezaji wa
Ilani ya chama cha Mapinduzi hususani kwenye Miundo mbinu na shughuli za
Kiuchumi."Kitapataje
kibanda cha Uchohoroni DAWA ambazo Serikali haina???" Kuna watumishi wa
serikali wanaiba dawa na kuwaelekeza wananchi kwenda Kuzinunua kwenye
Maduka yao ya Dawa.Mwigulu Nchemba amesema wakati umefikwa kwa
Watanzania kuwa walinzi wa mali za Umma,Kuchukua hatua kwa vitendo dhidi
ya wakwamisha maendeleo.Picha imecgukuliwa Korogwe Mh:Mwigulu
Nchemba akiagana na Wananchi wa Korogwe Mjini mara baada ya Kuhitimisha
ziara yake aliyoifanya kwa Mkoa wote wa Tanga kwa siku moja,Lengo
likiwa kueleza kuhusu utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi.
No comments:
Post a Comment