Tuesday 16 June 2015

VIDEO NA PICHA,MWIGULU ASUBIRIWA HADI USIKU NA WANAKIGOMA ILIWAMDHAMINI KUELEKEA URAIS WA JMT

Ndugu Mwigulu Nchemba mgombea Urais ndani ya CCM akionesha Orodha ya WanaCCM waliomdhamini mkoa wa Kigoma hii leo.Mwigulu Nchemba akisalimiana na WanaCCM walioamua kwa dhati kumdhamini iliaweze kupitishwa na Chama cha Mapinduzi kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Baadhi ya Wadhamini wa Mwigulu Nchemba hapa Kigoma,Wadhamini hawa wametumiza Zaidi ya Masaa 7 kumsubiri Mwigulu Nchemba aliyekuwa akitokea Mkoa wa Kagera.Awali walitangaziwa kuwa Mwigulu atawasili saa 7 Mchana,Kutokana na sababu zisizozuilika za barabarani,Mwigulu Nchemba aliwasili majira ya Saa 1 Jioni na kukutana na Wadhamini hao.Jambo ambalo limeonesha kuwa ni Uvumilivu wa hali ya Juu,na niwazi wadhamini hawa wanampenda Mwigulu awe kiongozi wao.Mwigulu akikabidhiwa orodha ya WanaCCM waliomdhamini kwa mkoa wa Kigoma.Mwigulu akiwa amempakata mototo wa Mwanaccm huyu(Kulia) ambaye ameamua kumdhamini Mwigulu Nchemba katika safari yake ya Kuwania kuteuliwa na CCM awe mgombea Urais wa JMT.

VIDEO MWIGULU ALIPOKUWA AKIWASILI UKUMBINI KUKUTANA NA WADHAMINI WAKE

No comments:

Post a Comment