Monday 31 August 2015

MWIGULU NCHEMBA AWAONYA WATANZANIA KUTOWAUNGA MKONO WAGOMBEA URAIS WENYE REKODI ZA KUPIGA DILI

Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Mh.J.P.Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Songea Mjini hii leo wakati wa mkutano wa kampeni Uliofanyika Uwanja wa Majimaji -Songea Mjini.Mbali na kuomba kura kwaajili ya Mbunge huto wa CCM,Mh;magufuli pia amewasisitiza Wananchi wa Songea na Mkoa wa Ruvuma kuwa anataka kuunda serikali ya "KAZI TU" ,Hivyo anaomba kura za kutosha kwa Madiwani,Wabunge na za Urais za kutosha ili aweze kuwa na serikali Imara ya Chama cha Mapinduzi itakayofanya kazi kwa niaba ya Watanzania wote.Mh;Magufuli akisalimiana na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mh.Mwigulu Nchemba aliyeshiriki tukio la kampeni hapa Songea Mjini.Mwigulu Nchemba ambaye ni Mgombea Ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza na Wananchi wa songea Mjini,Amewaomba Watanzania wote kuwamakini sana na wagombea waigizaji wakati huu wa kampeni za Urais,Taifa linahitaji kiongozi Mchapa kazi na mwenye nia ya dhati ya Kulitumikia Taifa letu.Watanzania wote wanatambua kati ya wagombea wote ni yupi anarekodi ya Uchapa kazi wakati wote alipokuwa serikalini ambaye ni Magufuli ,Wakati huohuo wagombea wengine wanarekodi za kutiliwa mashaka tangu wakiwa na miaka 40 hivyo hawafai kuwa watumishi wa Umma.
Mwigulu Nchemba alikwenda mbali Zaidi kuwa,Kuna wagombea Urais wamezungukwa na MAGENGE ya WAPIGA DILI tu ambao wanageuza mchakato wa Urais kama sehemu yao ya kujiandaa kwenda kuiba mali za Umma.Hivyo huu sio wakati wa watanzania kujiuliza mara mbili nani anatakiwa kuwa Rais,Jibu ni J.POMBE MAGUFULI.
Picha na Sanga Jr.

No comments:

Post a Comment