Friday 11 September 2015

TASWIRA YA MAELFU YA WANANCHI WA MUSOMA WALIVYOJITOKEZA KUIINGA MKONO CCM,MWIGULU AELIMISHA KUHUSU KAULI YA MWALIM NYERERE

Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi Mh.Jonh Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Musoma Mjini jioni ya leo wakati wa Mkutano wa Kampeni za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Magufuli amesisitiza/ameomba wananchi wa Musoma kuchagua wagombea wa Chama cha Mapinduzi kwasababu ndicho chama chenye Ilani Bora na yeye amejipanga kuhakikisha anatatua kero zinazowakabili Wananchi wote wa Tanzania bila kubagua.Sehemu ya Maelfu ya wananchi wakifuatilia Mkutano wa kampeni wa Chama cha Mapinduzi hapa Musoma mjini hii leo.Wajumbe wa kamati ya Ushindi Ndg.Makongoro Nyerere na Mwigulu Nchemba wakifurahia jambo wakati wa Mkutano huo.Mgombea Ubunge Jimbo la Musoma Mjini Ndg.Vedasto Mathayo akiomba kura kwa wananchi wake,Kubwa amesisitiza kuongoza kazi ya utatuzi wa kero ya Maji,Barabara na Afya kwa wananchi wa Musoma Mjini.Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Mpya Mh.Jaji Warioba akibadilishana mawazo na Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi Ndg.J.Pombe MagufuliWarioba akizungumza na Wananchi wa Musoma,Amebainisha kuwa moja ya vitu muhimu kwenye Katibu Mpya ilikuwa ni Swalala Maadili kwa Viongozi na Mamlaka ya Rais.Hivyo kwakuwa UKAWA walikuwa wanapigia kelele swala hilo,Hivi sasa hao hao UKAWA wamepoteza uhalali wa kuzungumzia maadili ya Viongozi kwasababu KIONGOZI ASIYENAMAADILI ndiye wamemsimisha kugombea Urais,Pia huyohuo Mgombea wao ameonesha wazi wazi kuwa Utawala wa sharia kwake hautakuwepo kutokana na Kauli zake za kuachia watu walikwisha hukumiwa.Mwigulu Nchemba ambaye ni Mjumbe wa kamati ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi ameendelea kuwaelimisha Watanzania namna UKAWA wanavyopotosha Umma kuhusu Kauli za Baba wa Taifa. Nanukuu"Ni kweli Baba wa Taifa Mwl.Nyerere alisema Watanzania wasipoyapata Mabadiliko ndani ya CCM watayatafuta NJE ya CCM."
Kauli hiyo ya Kutafuta Mabadiliko nje ya CCM ambayo ilisemwa na Baba wa Taifa ilijikita kwenye Mambo makuu 4 ambayo Watanzania wasipoyaona ndani ya CCM watakwenda kuyatafuta nje ya CCM.
Jambo la kwanza ni RUSHWA,Mwl.Nyerere alisema,Watanzania wanahitaji kiongozi anayeweza kukemea Rushwa bila kuona aibu,Rais aweze kuwambia Jamaa zake kuwa Rushwa ni hatari kwa Ustawi wa Taifa letu.Hivyo Watanzania wasipopata mtu anayepinga Rushwa ndani ya CCM watakwenda kumtafuta nje ya CCM.Swali kwa uchaguzi huu wa mwaka 2015,Mtu anayepinga RUSHWA yupo ndani ya CCM au Nje ya CCM?? Jibu ni yupo ndani ya CCM na yule mwenye sifa ya kula Rushwa na kuiba mali za Umma yupo NJE ya CCM.Hivyo Watanzania wanatakiwa kuiingua Mkono CCM na sio hao wengine.
Jambo la pili MUUNGANO, Mwl.Nyerere alisema Kiongozi Mkubwa kama Rais ni lazima autetee Muungano wa Nchi yetu.Hivyo Watanzania wasipopata Mgombea ndani ya CCM anayeweza kuutetea Muungano wetu,Watakwenda NJE ya CCM kumtafuta mtu anayeweza kutetea Muungano wetu. Swali,Kati ya CCM na Wagombea wengine ni Mgombea yupi anasera za kuutetea Muungano wetu??Rejea kauli ya Mwl.Nyerere kuwa serikali tatu(3) ni kuua Muungano wetu.
Jambo la tatu ni UDINI na UKABILA,Mwl.Nyerere alisema ,Kiongozi wa Taifa kubwa kama Tanzania ni lazima adumishe Ummoja kwa kuzuia Udini na Ukabila.Hivyo Watanzania wasipopata Mgombea Urais anayeweza kukemea Udini na Ukabila bila kuuonea haya watakwenda nje ya CCM kutafuta mtu anayekemea Udini na Ukabila.Swali,Kwa wagombea wa sasa kwenye Uchaguzi huu 2015 ni Mgombea yupi anaeneza UDINI na Ukabila na Yupi anakemea Udini na Ukabila??Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mgombea Urais Ndg.J.Pombe Magufuli.Mgombea Ubunge jimbo la Bunda Mjini Mh.Masato Wassira akizungumza na Wananchi wa Musoma na kuwaomba waachane na udanganyifu unaofanywa na Viongozi wa UKAWA kuhusu Mabadiliko.Amesema UKAWA wanataka kuwaletea Mabadiliko ya Kurudisha nyuma maendeleo.Bi.Shy-Rose Bhanji ambaye ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na Kada mtiifu wa chama cha Mapinduzi akiteta jambo na Mwigulu Nchemba.Comrade Makongoro Nyerere akiwaambia Wananchi wa Musoma kuwa Mgombea wa UKAWA hashafishiki hata kwa dodoki,Hivyo kazi anayoifanya Sumaye haitaleta Matunda.
 
Picha na Festo Sanga Jr.

No comments:

Post a Comment