Tuesday, 22 December 2015

MWIGULU NCHEMBA ATUA KAGERA KUWATAFUTIA MALISHO WAFUGAJI,WIZARA YA MALI ASILI YAAHIDI KUSAIDIA WAFUGAJI

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akiwasili eneo la mkutano uwanja wa Mnadani wilayani Ngara kuzungumza naWafugaji/wakulima mapema hii leo.Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Naibu Waziri wa Mali asili Mh.Ramo Makani ambaye waliongozana naye kwenye mkutano huo kama wadau wa wafugaji kwenye mapori yanayosimamiwa na Mali Asili.Mwigulu Nchemba akizungumza na Wafugaji/Wakulima waliokusanyika kutoka wilaya ya Ngara,Muleba,Karagwe n.k
 
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akimuomba maeneo ya Malisho ya wafugaji yaongezwe kutoka mapori ya akiba ambayo kwa sasa yanawezwa kutumiwa na wafugaji wa mkoa wa kagera.
Mh.Ramo Makani akimhakikishia Mh.Mwigulu Nchemba kuwa Wizara ya Mali Asili itafanya kazi bega kwa bega na Wafugaji na wakulima hususani kwenye maeneo yanayozunguka hifadhi za Mali asili na wanyama.
 
Mapema leo Desemba 22/2015, Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba amekutana na Wananchi wafugaji na wakulima wa wilaya za Ngara,Karagwe,Biharamulo,Kyerwa n.k Mkoani Kagera kuzungumza nao adhima yake ya kutatua tatizo la malisho kwa wafugaji wanaozunguka mapori tengevu yanayopatikana Mkoa wa Kagera.
Katika mkutano uliofanyika Uwanja wa Mnadani (Benaco) Ngara,Mwigulu Nchemba amesikiliza changamoto zinazowakabili wafugaji kupitia Chama cha Wafugaji wa kanda ya Ziwa (CHAWAKAZI) kilichosajiliwa mwaka 2002 kinachojumuisha wafugaji kutoka Kahama,Bukombe,Geita,Chato,Ngara,Muleba n.k.,Changamoto kubwa ambayo wafugaji wameiwasilisha kwa Mh.Waziri ni uonevu na unyanyasaji unaofanywa na askari wa wanyamapori wanaolinda Mapori ya akiba ya Burigi,Kimisi,Rumanyika,Muyowosi na Kigosi.Askari wanyamapori wanashutumiwa kujihusisha na utesaji wa ng'ombe wanaokamatwa maeneo karibu na mapori hayo,Ulipishwaji wa faini zisizohalali kwa madai ya ng'ombe kuingia kwenye hayo mapori.
Zaidi,Wafugaji wameomba serikali iwapatie maeno ya mapori ambayo kwa sasa yanaweza kuwa sehemu ya lanchi ndogo za wafugaji.Pia wameoimba serikali iachane na operation ya kuwaondoa wafugaji kutoka kwenye maeneo yanayotumika kuchunga ng'ombe katika pori la Burigi.
Akitoa majawabu ya changamoto hizo,Mwigulu Nchemba amewasisitiza wananchi mambo makuu mawili(2).Kwanza watambua kuwa serikali imedhamiria kutatua migogoro yote inayoikabili sekta ya ufugaji,kilimo na uvuvi,Hili linakwenda sambamba na agizo la Mh.Rais  J.Magufuli kuwa wakulima na wafugaji wapatie suluhisho la kudumu,Pili amewaomba wafugaji na wakulima kuheshimu hifadhi zilizotengwa ilivizazi vijavyo viwezekunufaika nazo.Kwa upande wa maeneo ya malisho,Mwigulu Nchemba amemuomba Naibu Waziri wa Mali Asili kupitia ofisi yake iangalie uwezekano wa kuyapitia upya mapori tengevu ili baadhi wapewe wafugaji na wakulima kwa shughuli zao.
 
Akioneshwa kuguswa na changamoto za wafugaji wa mkoa wa Kagera na Tanzania yote,Naibu waiziri wa Mali Asili ametangaza kusitishwa kwa operation za kuwaondoa wafugaji kwenye maeneo wanayochungia mifugo yao,Pilia ameahidi kupitia ofisi yake itafanya haraka iwezekanavyo utaratibu unaoendelea wa kupitia mapori 17 ilikutoa maeneo kwa watu waweze kufanya shughuli zao(Kilimo,Mifugo n.k)
Mh.Ramo kupitia hadhara hiyo amelaani kitendo kilichofanywa na watu wanaodaiwa kuwa ni kutoka Mali Asili waliofyeka ekari 150 za mahindi wilaya ya Mbozi."Ni jambo lisilokubalika kabisa,na kupitia mkutano huu naagiza kama kuna wakulima wamelima eneo ambalo linadhaliwa ni hifadhi waachwe hivyohivyo hadi hapo mazao yatakapo komaa na utaratibu mwigine utakapotolewa"
Lakini pia,Mh.Ramo amewaomba askari wanyamapori kuzingatia maadili ya kazi yao,kwa wale baadhi wanaojihusisha na utesaji,Unyanyasaji na kujipatia fedha haramu kwa kukamata mifugo au wakulima waache mara moja,Serikali inakwenda kuchukua hatua kuhakikisha askari wote wanafanya kazi kwa kuheshimu sharia za nchi.
Imeandikwa/Picha na Festo Sanga (R)

No comments:

Post a Comment