Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kujenga moja ya nyumba
ya waalimu katika shule ya sekondari ya Ikuti iliopo katika kata ya
Ikuti,Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya mapema leo,akiwa sambamba na Ujumbe
wake hawapo pichan,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na
Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Asharose Migiro.Kinana na
Ujumbe wake wako ziarani Wilayani Rungwe Magharibi mkoani Mbeya,ambapo
kesho watakuwa wilaya ya Ileje kutekeleza Ilani ya chama,kukagua miradi
ya chama na wanachi sambamba na kujua na kutatua matatizo yao kwa namna
moja ama nyingine.
Wakienda kukagua moja ya bweni la kulala wanafunzi wa shule hiyo ya Ikuti
Katibu
wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa ,Asharose Migiro wakielekea
kuonana na balozi balozi wa shina la Kitonga,ndani ya kijiji cha
Ikuti,Bwa.James Mbasi ,pichani nyuma anaefuatia ni Katibu wa NEC,
Itikadi na Uenezi Nape Nnaupe
Katibu
Mkuu wa CCM,pili kushoto,Ndugu Abdulrahman Kinana na wajumbe wake
wakielekea kuonana na balozi wa shina la Kitonga,ndani ya kijiji cha
Ikuti,Wilayani Rungwe mapema leo.
Pichani
ni Katibu Mkuu wa CCM pichani kati,Ndugu Abdulrahman Kinana akikata
utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa kituo cha kuzalisha umeme kilichopo
kwenye zahati ya Ikuti,katika kijiji cha Ikuti wilayani Rungwe mkoani
Mbeya.
Kada maarufu wa CCM,Richard Kasesela akipiga ngoma ya asili ya kinyakyusa iitwayo Lipenenga.
Baadhi
ya vijana mbalimbali wakiwa juu ya miti wakifuatilia mkutano wa
hadhara,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa
akihutubia jioni ya leo kwenye kijiji cha Ikuti.
Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya kimataifa,Asharose Migiro akizungumzaa mbele ya wakazi wa kijiji cha Ikuti mapema leo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnaupeakizungumzaa mbele ya wakazi wa kijiji cha Ikuti mapema leo,Wilayani Rungwe.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wakazi wa kijiji cha Ikuti mapema leo,kwenye mkutano wake wa hadhara .
Mbunge
wa viti maalum mkoa wa Mbeya,Dkt Mary Mwanjelwa akifafanua jambo kwa
wakazi wa kijiji cha Ikuti mapema leo,Mbunge huyo pia aliwataka akina
mama kujiunga katika vikundi vya ujasiliamali,ili kurahisishiwa kupata
mikopo ya kuendeleza miradi yao ambayo wataianzisha katika suala zima la
kujikwamua na ugumu wa maisha,
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wafanyabiashara wa ndizi katika
soko la Iponjora,Wilayani Rungwe,Kinana aliwaasa wafanyabiashara hao
kutokuwa na tamaa ya kuuza biashara yao hiyo ya ndizi kwa bei ya
kutupa,badala yake waachane na watu wa kati,wafanye biashara yao kwa
faida na si kuwanufaisha wafanyabiashara wakubwa,ambao hawajui ugumu wa
kilimo cha zao hilo,Kinana katika kuwaongezea kasi ya biashara yao ya
ndizi aliwachangia kiasi cha shilingi laki moja
Katibu
NEC,Siasa na Mahusiano ya kimataifa,Dkt Asharose Migiro akizungumza na
wafanyabiashara wa ndizi katika soko la Iponjora,Wilayani Rungwe,mkoani
Mbeya.
Wakazi wa kijiji cha Ikuti wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe mara baada ya kuusimamisha msafara wake.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wakazi wa kijiji cha
Lupando,Kata ya Masoko Wilayani Rungwe mapema leo,Kinana alizungumza
mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kutatua tatizo sugu la Maji na
Barabara katika kijiji hicho,alichozaliwa Mbunge wa jimbo la Rungwe
Magharibi,Mh.Dkt David Mwakyusa.Aidha kinana aliitahadharisha Serikali
katika suala zima la kuitaka Serikali iache urasimu na umangimeza katika
mipango ya maendeleo kwa Wananchi,kwa sababu Urasimu na umangimeza huo
huwanufaisha zaidi wanaoshikilia fedha za miradi hiyo wakati wananchi
Wanaumia na kuteseka kwa kukosa huduma muhimu mbalimbali.
Mbunge wa jimbo la Rungwe Magharibi,Mh.Dkt David Mwakyusa,akizungumza
na wakazi wa kijiji cha Lupando,Kata ya Masoko Wilayani Rungwe mapema
leo kuhusiana na kero mbalimbali zinazowatatiza wakazi hao,ikiwemo suala
la maji na barabara sambamba na tatizo la bei ya zao la ndizi kutoka
kwa wakalima kwenda kwa wafanyabiashara.
Mbunge wa jimbo la Rungwe Magharibi,Mh.Dkt David Mwakyusa akisalimiaa na Katibu
NEC,Siasa na Mahusiano ya Nje,Dkt Asharose Migiro mara baada ya
kukutana katika kijiji cha Lupango,Wilayani Rungwe,ambapo Ndugu Kinana
aliwahutubia wakazi wa kijiji hicho.
Pichani
shoto ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya,Dkt Mary Mwanjelwa akiwa
na Katibu NEC,Siasa na Mahusiano ya kimataifa,Dkt Asharose Migiro
walipokuwa wakielekea kukagua jengo la bweni la kulala wanafunzi wa
shule ya sekondari ya Ikuti,Wiayani Rungwe mkoani mbeya leo.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wakereketwa wa shina la vijana
waendesha boda boda katika soko la Kiwira,ambapo Ndugu Kinana
aliwachangia kiasi cha fedha shilingi milioni tano kwa ajili ya
kujiendeleza na kuwapa uwezo wa kujikopesha wenyewe katika suala zima la
kujikwamua na suala zima la umasikini,hasa ikifahamika kuwa tatizo la
ajira kwa vijana limekuwa kubwa.
Pichani shoto ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya,Dkt Mary Mwanjelwa akiwa amepozi na mdau.
No comments:
Post a Comment