Sunday 17 November 2013

KINANA: VYAMA VYA USHIRIKA VITETEE WAKULIMA NA SI KUWAKANDAMIZA

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Vita Kawawa Mbunge wa jimbo la Namtumbo Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma mara baada ya kumpokea kwenye kata ya Mchomoro, Abdulrahman Kinana yuko katika ziara ya kikazi ya mikoa ya Ruvuma, Mbeya na Njombe ambapo ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wakikagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzina kusikiliza matatizo ya wananchi ikiwa ni pamoja na kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, Katika ziara hiyo ya Wilaya za Tunduru na Namtumbo wananchi wamelalamikia kuhusu bei ya zao la Korosho ikiwa ni pamoja na Tumbaku, lakini pia wakalalamikia suala zima la Mbolea, ambapo Mbunge wa jimbo la Namtumbo Vita Kawawa ametuhumu baadhi ya viongozi wa vyama vha ushirika na ofisa ushirika wa mkoa huo kuwabambikizia madeni wakulima wa tumbaku kupitia ruzuku ya mbolea ambapo makadirio ya mbolea inayohitajika kwa wakulia huongezwa kinyemela na wananchi kuachiwa mzigo wa kulipa madeni ambayo hayawahusu jambo ambalo linawatesa wakulima wa tumbaku na kuwaacha wakiwa hoi. kiuchumi 3 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kulia akipata kifungua kinywa nyumbani kwa mwenyekiti wa shina ndugu Hussein Rwambo wa pili kutoka kulia katika kata ya Mchomoro, kulia ni Vita Kawawa Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, Kushoto aliyekaa ni Dr. Asga Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na aliyesimama mlangoni ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi. 4 
Hili ni jengo la Utawala la hospitali ya Wilaya Namtumbo. 8 
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika katika moja ya mikutano. 15 
Mmoja wa wananchi akitoa kero za wakulima wa zao la Tumbaku kwa niaba ya wananchi. 16 
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mh. Vita Kawawa akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara mjini Namtumbo, mkutano huo umefanyika kwenye uwanja wa Taifa.

No comments:

Post a Comment