ARUSHA, Tanzania
Mkutano
wa pili wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) kuhusu masuala ya Amani
na Usalama utafanyika mjini Bujumbura, Burundi kati ya Novemba 13 na
15, mwaka huu.
''Mkutano
huo utatoa fursa ya majadiliano kuhusu juhudi za kujenga amani,kuzuia
migogoro na ufumbuzi na pia kubadilishana uzoefu wa aina hiyo kutoka
jamii nyingine,'' alisema Charles Njorege, Naibu Katibu Mkuu wa EAC,
anayeshughulikia Shirikisho la Kisiasa, katika taarifa kwa vyombo vya
habari.
Aliongeza
kwamba mkutano huo utahudhuriwa na wajumbe wapatao 150 wakiwemo
wataalamu wa amani na usalama,mashirika ya kiraia,viongozi wa
dini,mawaziri, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali,wanasiasa,
vijana,waandishi wa habari na wizara za mamboya EAC.
Kwa
mujibu wa ofisa huyo wa EAC, wajumbe watajipata na kubadilishana
maarifa kwa lengo la kujifunza na kuboresha kuzuia migogoro na kuipatia
ufumbuzi na pia kusaidia kupata mwelekeo wa shughuli za siku za usoni
katika kanda.
Kauli
mbiu katika mkutano wa mwaka huu ni : Kujenga utamaduni wa majadiliano
na kuvumiliana katika kuzuia migogoro na kuishi kwa pamoja kwa amani.''
Pamoja
na mambo mengine wajumbe wanatarajiwa kufanya tasmini ya changamoto za
amani na usalama inazozikabili jamii,uzoefu uliopita,njia bora zaidi ya
kuzishughulikia na kubainisha hatua za kuweza kuzichukua ili kukuza
majadiliano, kuvumiliana na kuishi kwa pamoja kwa amani.
Mkutano huo utatanguliwa mafunzo kwa waandishi wa habari 25 kutoka nchi wanachama wa EAC kuhusu amani na kuripoti taarifa nyeti.
No comments:
Post a Comment