Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhani Madabida akifungua semina
ya siku 2 iliyoshirikisha Chama Cha Mapinduzi na Chama rafiki cha
Kikomunisti cha China CPC,katika hoteli ya Courtyard mjini Dar es
Salaam, Semina hiyo ilikuwa mahususi katika Kuvijengea Vyama Uwezo na
Umuhimu wa Vijana katika vyama.
Naibu Mkurugenzi
wa CPC katika masuala ya Kimataifa Ndugu An Yuejun akitoa salaam za
shukran kwa niaba ya wajumbe wenzake kabla ya kuanza kwa semina ya siku
mbili iliyoshirikisha CCM na CPC kutoka China.
Profesa
Song Li akitoa elimu juu ya masuala mbali mbali ya kiuchumi ikiwa
mipango iliyofanywa na CPC tangu kuanza kwake katika kuboresha na kukuza
uchumi wa China.
Katibu Msaidizi
Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Ndugu Anamringi Macha
akibadilishana mawazo na Makamu Mkurugenzi katika masuala ya Kimataifa
wa CPC Ndugu An Yuejun mara baada ya kumaliza semina kwa siku ya kwanza.
Naibu Katibu
Mkuu wa Umoja wa Wanawake (Zanzibar) Salama Aboud na Naibu Katibu Mkuu
wa Umoja wa Wanawake Bara wakifurahia jambo na Naibu Mkurugenzi wa
masuala ya kimataifa wa CPC Ndugu An Yuenjun.
Katibu wa Mkoa
wa Vyuo Vikuu CCM Ndugu Christopher Ngubiagai akitoa mada juu umuhimu wa
vijana katika CCM na matatizo yanayowakabili vijana wengi wa Tanzania
na kusini mwa jangwa la Sahara katika semina ya siku mbii iliyoanza
tarehe 31 Oktoba na kuhitimishwa tarehe 1 Novemba katika hotel ya
Courtyard jijini Dar es Salaam na kushirikisha vyama viwili marafiki CCM
na CPC kutoka China.
Suleiman Mwenda
kutoka Idara ya Itikadi na Uenezi akielezea namna internet inavyofanya
kazi katika kufikisha ujumbe hasa kwa vijana na pia hatua ambazo
serikali inazichukua katika kuboresha na kuzuia upotoshaji ama matumizi
mabaya ya internet.
Gift Msuya
kutoka Mkoa wa Vyuo Vikuu akifafanua masula mbali mbali yanayohsu mkoa
huo wa vyuo vikuu wakati wa semina ilyoshirikisha CCM na CPC kutoka
China.
Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Dar es Salaam ndugu Ramadhani Madabida akitoa mada juu ya
mfumo mzima wa Chama Cha Mapinduzi katika semina ya siku mbili
iliyoshirikisha CCM na CPC kutoka China.
Katibu Mkuu
Msaidizi wa Idara ya Itikadi na Uenezi akiuliza swali linalohusu ubora
wa bidhaa kutoka China wakati wa semina ya siku mbili iliyohushisha CCM
na CPC kutoka China.
Makamu
Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Mboni Mhita akielezea umuhimu wa Umoja wa
Vijana wa CCM katika semina ya siku mbili iliyofanyika katika Hotel ya
Courtyard na kushirikisha vyama viwili marafiki CCM na CPC kutoka China.
Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhani Madabida akiwa kwenye picha ya
pamoja na viongozi kutoka Chama rafiki cha Kikomunist cha China pamoja
na Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam ndugu Abdilah Mihewa na
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Ndugu Salum Madenge
No comments:
Post a Comment