- AFANYA KIKAO NA WANANCHI
- WANANCHI WAELEZA KERO ZAO NA WAMILIKI WA MGODI WA NORTH MARA,POLISI,MKUU WA WILAYA,KIKOSI KAZI(TASK FORCE),UKIUKWAJI WA MIKATABA ,KUSITISHWA KWA MALIPO YA ADA ZA WANAFUNZI NA MAJI YENYE KEMIKALI KUTOKA MGODINI NA KUINGIA KWENYE MITO.
- AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akifafanua jambo wakati wa kikao maalum
cha ndani na wakazi wa eneo la Nyamongo, ambapo wananchi wa eneo hilo
walikuwa wakieleza kero zao na wamiliki wa mgodi wa North Mara .
Ndugu
Elizabeth Malembela akielezea jinsi utaratibu ulivyombovu wa
kuwahamisha na kuwalipa fidia wakazi wanaoishi kando kando ya mgodi wa
North Mara.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisikiliza kwa makini malalamiko
ya wananchi wa Nyamongo juu ya ukiukwaji wa utaratibu na mikataba baina
ya wawekezaji na Wanavijiji.
Mkuu wa
Wilaya ya Tarime Ndugu John Henjewele akiwaelezea wakazi wa Nyamongo
kazi za kikosi kazi (Task force) katika kurahisisha shughuli za
kutathimini ardhi na kuchukua malalamiko ya wananchi dhidi ya wawekezaji
wa mgodi wa North Mara.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia moja ya eneo linaloaminika
kutiririsha maji yenye kemikali kutoka kwenye Mgodi wa North Mara kwenda
kwenye mto Mara na kuhatarisha afya za wananchi.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia kwa karibu kabisa maji ya
kemikali kutoka machimbo ya mgodi wa North Mara kuelekea mtoni.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma jiwe la msingi la ofisi ya
Kikundi cha Bodaboda Nyamongo mara baada ya kuzindua ofisi hiyo.
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Ndugu Amos Sagara Nyabikwi akihutubia
wakazi wa Nyamongo wakati wa mkutano wa hadhara ambao Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye aliwaelezea wananchi wa eneo hilo hatua za
awali za kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao zilivyoanza.
Mkurugenzi wa
Kushughulikia Malalamiko dhidi ya Jeshi la
Polisi,Magereza,Uhamiaji,Zimamoto na Uokoaji Ndugu Agustine D. Shio
akihutubia wananchi wa Nyamongo na kuwaambia amesikia malalamiko yao
dhidi ya Jeshi la Polisi na atalifanyia kazi mapema iwezekanavyo na haki
zitapatina.
Sehemu ya Wakazi wa Nyamongo wakisikiliza kwa makini hotuba ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi nape Nnauye.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nauye akihutubia wakazi wa Nyamongo wilayani
Tarime na kuwaelezea jinsi alivyoanza rasmi kazi ya kutafuta ufumbuzi wa
matatizo yanayowakabili wananchi wa Nyamongo
No comments:
Post a Comment