

Mh.Mwigulu Nchemba akiwa Shinyanga pia alifanikiwa kufanya vikao vya ndani na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi WIlaya ya Shinyanga mjini na Mkoa,Pia alitumia muda wake kukutana na Mabalozi wa wilaya ya Shinyanga mjini.
Pamoja na mambo mengine,Mh.Mwigulu ambaye ni Naibu Katibu Mkuu aliwaomba viongozi wa CCM wilaya kusimamia miradi ya maendeleo vizuri(Ujenzi wa Zahanati,Shule,matundu ya Vyoo ya wanafunzi,.Soko,Jengo la NSSF) ambayo yote hayo ni jitihada za Mh.Masele kwa wananchi wake wa Shinyanga Mjini.
Naibu Katibu Mkuu kupitia vikao vyake vya ndani na kwenye Mkutano wa hadhara amewasisitiza Wananchi wa Shinyanga Mjini kumpatia ushirikiano Mh.Masele katika shughuli zake zote za maendeleo,Ikumbukwe Mh,Masele ni Naibu wa Wizara ya Nishati na Madini,Hivyo basi anakazi nyingi za serikali na za jimboni kwake,Wananchi na viongozi wa Chama na Serikali wanatakiwa kuhakikisha wanampatia Mbunge huyo Ushirikiano wa kutosha ilikuhakikisha Ilani ya chama cha Mapinduzi inafanikiwa vizuri.
Katika hali isiyoyakawaida Madiwani wawili wa kata zinazongozwa na CHADEMA Shinyanga Mjini wamekalia mifuko 200 ya Cement aliyotoa Mh.Masele kwaajili ya Ujenzi wa Soko na Zahanati.Tukio hilo limetokea wakati Mh.Masele miezi 3 iliyopita aligawa mifuko ya CEMENT kwa kata zake zote kulingana na Mahitaji yao,Katika kata ambazo CHADEMA wanaongoza waliomba mifuko ya CEMENT 100 kila kata kwaajili ya Ujenzi wa SOko na Zahanati,Vivyo hivyo kwa Kata za CCM ikiwamo ya kambarage walipewa mifuko 100 kwaajili ya ujenzi wa Zahanati na matundu ya Choo ya shule.
Huku Kata zingine zinazongozwa na CCM zikiwa zimekamilisha ujenzi huo kwa asilimia zaidi ya 80,kata zinazongozwa na CHADEMA mifuko imepatikana Nyumbani kwa madiwani hao bila kutoa sababu za Msingi ni kwanini wameshindwa kujenga maeneo husika kutokana na maombi yao.
Katika ziara yake Mh.Masele ameagiza Madiwani wa kata husika wawajibishwe na wananchi wao kwa kukwamisha miradi ya maendeleo kwa maksudi(hujuma).Vile vile amejitolea kusaidia kila kata kumalizia ujenzi wa Zahanati,Soko na matundu ya Shule,Kwa awamu ya kwanza amekuja na Nondo kwaajili ya Madirisha na milango na ameshaanza kugawa kwa kata zile zilizokamilisha zoezi la ujenzi wa miradi yao isipokuwa zile za CHADEMA.
Wilaya ya Shinyanga mjini inajumla ya kata 17 na kata 6 zinaongozwa na Upinzani.
No comments:
Post a Comment