Sunday, 8 December 2013

WATANZANIA JIJINI NEW YORK NA VITONGOJI VYAKE WALIVYOSEREBUKA MIAKA 52 YA UHURU WA TANGANYIKA



 Joy na Maurus wakiwaongoza watanzania kuimba wimbo wa Taifa.
Mhe. Balozi Tuvako Manongi akizungumza  machache.
Sehemu  ya Wageni
Mhe. Balozi Tuvako Manongi akikata keki wengine 
onesho la mavazi yaliyobeba  maudhui ya utamaduni wa mtanzania  yalitia fora sana
picha ya kuchora
Watanzania wakiserebuka.
 
Jumuiya ya Watanzania Jijini New York na Vitongoaji vyake jana Jumamosi imesherehekea miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika, katika Hafla iliyojaa nderemo, shamrashamra zikiambatana na muziki, chakula, vinywaji na maonyesho ya nguo zilizokuwa na maudhui ya utamaduni na desturi ya mtanzania. Sherehe hizo zilitanguliwa na mchezo wa mpira wa miguu kati ya Timu ya New York na Timu ya ....... ambako timu ya New York iliibuka kidedea.

Mgeni Rasmi katika sherehe hizo zilifana kiaina yake alikuwa ni Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa, Balozit Tuvako Manongi ambaye alifuatana na Naibu wake Balozi Ramadhan Mwinyi na tukaungwa mkono na Balozi wa Somalia katika Umoja wa Mataifa . Watanzania hawa alisimama kwa sekunde Moja, kumukumbuka na kumwombea Marehemu Rais wa Kwanza wa Afrika ya Kusini Huru, Mzee wetu Nelson Mandera.

katika Salamu zake fupi alizozitoa kwa watanzania hao wa Jiji la New York na Vitongoji vyake, pamoja na kuishukuru Jumuia hiyo ya Watanzania kwa maandalizi mazuri ya sherehe hizo, Balozi Tuvako Manongi amewaasa watanzania hao kuendeleza na kujenga misingi ya utaifa, uzalengo, kupendana na kuheshimiana.

Akasema kila mtanzania anayohaki ya kuwa mfuasi wa chama chochote kile cha siasa, lakini jambo kubwa na la msingi linalowaunganisha watanzania popote pale walipo si itiakadi za vyama bali ni utanzania wao ambao umejengekea katika misingi ya utaifa, uzalendo, kuheshimiana, kupendana , kusaidiana ikiwa ni pamoja na kuitetea nchi yao.

Kwa upande wao, Jumuiya hiyo ya Watanzania katika Salamu zao kwa Serikali kupitia Balozi Manongi, wameomba suala la uraia wa nchi mbili lipewe umuhimu wa pekee katika mwenendo mzima wa mchakato wa Katiba mpya unaoendelea.

No comments:

Post a Comment