







Mh.Mwigulu
Nchemba amewasifu Wananchi kwa kuunganisha Nguvu zao na hatimaye
kujenga Soko,Pia amewaomba kuwa walitumie soko hilo kwa Ushirikiano
Mzuri wa wao kwa wao,Kujenga Jengo na Kuacha kulitumia si Jambo jema
kabisa kabisa.Mh.Mwigulu Nchemba amesema"Naiomba serikali na wote
wanaohusika na Ukusanyaji wa Kodi waangalie Viwango vya Ukusanyaji Kodi
kwa Wafanyabiashara wa soko hilo,Isije kuwa kunakuwa na Makato ya Jumla
bila kutofautisha mitaji ya Wafanyabiashara,haki itendeke kukusanya kodi
kutokana na Kiwango cha Biashara cha Mtu".
Mbali
na hilo Mh.Mwigulu amewataka Kamati ya Wananchi ilihohusika kwenye
Ujenzi wa Soko hilo,Kuhakikisha wanafanya utafiti wa Gharama za Umeme
unaotakiwa Kuwekwa kwenye Soko hilo,Yeye kama Mbunge wa Iramba anachukua
Jukumu la Kusimamia na kuhakikisha Umeme unawaka kwenye Soko hilo
ilikuwapa nafasi Wafanyabiashara kufanya shughuli zao hata Nyakati za
Usiku.
Hili ni Soko Kubwa la Pili
kuzinduliwa Eneo la Kiomboi,Mwaka jana wakati wa Mbio za
Mwenge.Mh.Mwigulu Nchemba pia alishiriki Uzinduzi wa Soko la Misigiri la
Wakulima.Soko lenye Ukubwa sawa na hili la Kiomboi.
No comments:
Post a Comment