Naibu Katibu Mkuu akizungumza na Ugeni Kutoka chama rafiki cha National Resistence Movement(NRM)Kutoka Uganda waliofika Kujifunza Mambo mbalimbali ya Kiuongozi/Kiutendaji ndani ya Chama cha Mapinduzi.
Naibu katibu Mkuu CCM-Bara Mh:Mwigulu akimkabidhi Kitabu/cha Mwongozo cha Chama cha Mapinduzi Kiongozi wa Serikali ya Uganda(NRM).
Naibu
Katibu Mkuu CCM-Bara Mh:Mwigulu Nchemba akimkabidhi Katiba Ndugu
Nnsiima Emmanuel Bigirwa Mchambuzi wa Mambo ya Siasa Kutoka Serikali ya
Uganda.
Mh:Mwigulu akimkabidhi kanuni za Uchaguzi zinazotumiwa na Chama cha Mapinduzi.
Ujumbe huu Kutoka NRM Wakifurahia Jambo kutoka Chama Cha Mapinduzi.
Viongozi
hawa Kutoka Uganda Wamefurahia sana Kupata Elimu ya namna Chama cha
Mapinduzi kinavyojiendesha,Ikumbukwe Uganda kwa Muda mrefu imekuwa
Ikiendesha siasa zake katika Mfumo wa Chama Kimoja,Ujio wa Vyama Vya
Upinzani umekuwa Changamoto kwa chama cha NRM hivyo wanatumia fursa
mbalimbali Kujifunza namna ya Kufanya siasa za Ushindani kama CCM
inavyofanya hapa Tanzania.Upande wa Kulia ni Hon. Nabulya Ssentongo
Theopista.
Mh:Mwigulu Nchemba akipokea Zawadi Kutoka Ujumbe wa Chama cha NRM-Uganda.
Mh:Mwigulu
Nchemba akitoa Maelezo namna Chama cha Mapinduzi kinavyofanya Kazi zake
na Muundo wa Uongozi Kuanzia Ngazi ya Shina hadi Tawi na Mfumo Mzima wa
Uchaguzi unavyoendeshwa ndani ya Chama cha Mapinduzi.
Hafla
hii imefungua Mlango Mkubwa zaidi wa Urafiki na Umoja kati ya Chama cha
Mapinduzi na Chama Kinachoongoza Serikali ya Uganda cha National
Resistence Movement Kutokana na Kuwekeana Malengo ya Kuendelea Kushirikiana Katika Uga wa Siasa na Nyanja zingine za Kiuchumi na Kijamii.
Picha/Maelezo na Sanga Jr
No comments:
Post a Comment