Thursday 22 May 2014

ZIARA YA KINANA WILAYA YA IKUNGI YAWATIA MOYO WA MAENDELEO WANANCHI.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia maharage mabichi yaliovunwa kutoka kwenye shamba la kampuni ya kilimo ya Singida ambao wanalima kwa kisasa umwagiliaje wa matone, kulia kwake anayempa maelekezo ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo ya kilimo Ally Mohamed.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdukrahman Kinana akiangalia bomba nyembamba zinazotomuka kumwagilia kwa matone kwenye shamba la kampuni ya kilimo ya Singida .
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kuandaa shamba katika shamba la maharage mabichi wilayani Ikungi mkoa wa Singida, shamaba hilo la kisasa ni mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa matone ambalo lipo chini ya Kampuni ya Kilimo ya Singinda (Singida Agriculture .co.ltd)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakishiriki kuweka maharage mabichi kwenye boksi tayari kwa kusafirishwa kwenda kwenye masoko,Maharage hayo yanalimwa kwa kilimo cha kisasa cha umwagiliaji wa matone mkoani Singida.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi madaftari kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu yaliyotolewa na umoja wa akina mama wa CCM wilaya ya Ikungi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wilayani Ikungi, Singida.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa darasa la shule ya msingi Unyaghumpi katika Jimbo la Singida Mashariki.
 Wanafunzi wa awali  shule ya msingi Unyaghumpi katika Jimbo la Singida Mashariki wakiwa wamekaa chini kwa kukosa madawati darasani, hii shule ipo kwenye jimbo la Mbunge Tundu Lissu ambaye inasemekana amezuia wananchi wake wasichangie kwenye miradi ya maendeleo.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisaidia kuvuna mtama na uwele kwenye shamba bibi mjane asiye na mtoto, Mayasa Mkhandi katika Kata ya Unyaghumpi, Jimbo la Singida Mashariki, mkoani Singida,wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. 
 Mlezi wa Mkoa wa Singida na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Ndugu Hadija Aboud akishiriki kuvuna mtama na uwele ,Ikungi mkoani Singida.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye eneo la mkutano wa hadhara katika tarafa ya Mungaa, Makiungu
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara ulofanyika  katika Kijiji cha Makiungu, wilayani Ikingu, Jimbo la Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu wa Chadema. Katibu Mkuu wa CCM aliwataka wananchi hao wafikirie zaidi kuhusu maendeleo ya jimbo lao na kuacha kuamini maneno ya viongozi wao wanaowazuia kuchangia maendeleo ya jimbo lao.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnaye akihutubia wakazi wa  Makiungu, tarafa ya Mungaa na kuwaambia wananchi hao wakati umefika wa kuwaomndoa viongozi ambao wanawazuia wananchi kuchangia maendeleo yao.
 Aliyekuwa kiongozi wa Chadema, Ismail Gwau, akitupilia mbali bendera ya CHADEMA mara baada ya kutangaza kujiunga na chama cha CCM,katika Mkutano huo wa hadhara.
  Ismail Gwau, akionyesha kadi mpya ya CCM mbele ya Kinana na kuashiria kujiunga rasmi na CCM,Ikungi mjini.
Wananchi wa Ikungi mjini wakila kiapo cha CCM.

No comments:

Post a Comment