Tuesday, 6 May 2014

TASWIRA:MAPOKEZI YA RIDHIWANI KIKWETE NA GODFREY MGIMWA CCM MAKAO MAKUU DODOMA

Makamu Mwenyekiti CCM-Taifa Philip Mangula akibadilishana Mawazo na Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara Mh:Mwigulu Nchemba na Mbunge wa Chalinze Mh:Ridhiwani Kikwete hii leo wakati wa hafla Fupi ya Kuwapokea Wabunge wapya wa Jimbo la Chalinze na Kalenga,Hafla imefanyika Makao Makuu ya CCM-Dodoma.Mh:Mwigulu Nchemb akimvisha Skafu huyu Mwimbaji baada ya Kuimba nyimbo ya hisia Kuhusu thamani ya Muungano na namna Wapinzani wanavyotaka Kuipeleka Nchi kwenye Utengano na Ubaguzi.
 Mh:Philip Mangula Makamu Mwenyekiti-CCM Taifa akizungumza na Wananchi waliofika Viwanja vya CCM Dodoma Makao Makuu wakati wa Hafla ya Kuwapokea Mh:Ridhiwani Kikwete na Mh:Godfrey Mgimwa.
Mangula ameonya Wana-CCM wanaofanya Kampeni kwenye Majimbo mbalimbali wakati Muda wa Kampeni haujafika,Amesema ni Kosa kwa Mtu yeyote anayejipitisha Kwa Wananchi kuomba ridhaa ya Kugombea Kupitia Chama cha Mapinduzi wakati muda haujafika,Ameomba Jimbo la Kalenga na Chalinze Wabunge wao wapewe nafasi ya Kutekeleza ahadi zao kwa Muda mfupi Uliobakia.Mbali na hilo Philip Mangula ameonya Makundi ndani ya Chama na Usaliti wakati wa Uchaguzi,Mwana-CCM Mtiifu hawezi Kukisaliti chama wakati wowote Ule,Hivyo Ikibainika Umesaliti Chama adhabu yake ni Kali sana.
Baadhi ya Vijana wa CCM-Dodoma Mjini wakipata Picha ya Pamoja na Mh:Mwigulu Nchemba.
 Mh:Mwigulu Nchemba akiongozana na First Lady Mama Salma Kikwete kuelekea kwenye Hafla ya Chakula kwenye Viwanja vya Royal Village Mchana wa leo wakati wa Kuwapokea Mh:Ridhiwani Kikwete na Mh:Godfrey Mgimwa.Burudani zinaendelea.
Mwimbaji Hafsa Kazinja akiwapa Burudani ya Mziki Mh:Mwigulu Nchemba na Wabunge wapya.
 Naibu katibu Mkuu-CCM Taifa Mh:Mwigulu NChemba akifurahia Jambo na Mbunge wa Chalinze Mh:Ridhiwani Kikwete.

Mh:Mwigulu Nchemba akiteta Jambo na Mbunge wa Kalenga Mh:Godfrey Mgimwa.
Dokii akitoa Burudani ya Mziki kwa Wananchi waliofika kwenye tukio hili.
Mh:Ridhiwani akimtambulisha Mke wake Bi.Ridhiwani.
 MH:Ridhiwani Kikwete akitoa neno la Shukrani kwa Wananchi wote na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi walioshiriki kwenye Mchakato mzima wa Uchaguzi hadi yeye kufikia hatua hii.
Huyu ndio Mama aliyemlea Ridhiwani Kikwete ndani ya CCM Tangu akiwa na Miaka 6 hadi hapa amekuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze.
Mh:Godfrey Mgiwa akimtambulisha Mke wake.
 Mh:Gofrey Mgimwa akitoa neno la Shukrani kwa Chama cha Mapinduzi na Viongozi wake kwa Kumfikisha hapa baada ya Mchakato Mzito wa Uchaguzi.
Mke wa Mh:Rais Jakaya Mrisho Kikwete-Mama Salma Kikwete akitoa Shukrani kwa Wananchi waliofika kwenye Hafla fupi ya Kuwapongeza Wabunge wapya Mh:Ridhiwani Kikwete na Mgimwa kwa Kuanza safari yao ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Picha/Maelezo na Festo Sanga.

1 comment: