Tuesday 28 October 2014

MWIGULU NCHEMBA AOKOA JAHAZI,AZUNGUMZIA HATUA ZINAZOCHUKULIWA KULIPA DENI MSD NA MIFUKO YA JAMII.

Mwigulu: Tutalipa deni la Sh8.4 Tril

Serikali imesema inaandaa utaratibu wa jinsi ia kulipa madeni inayodaiwa na taasisi za hifadhi ya

Dar es Salaam. Serikali imesema inaandaa utaratibu wa jinsi ia kulipa madeni inayodaiwa na taasisi za hifadhi ya jamii pamoja na Bohari ya Dawa (MSD).

Mifuko hiyo inaidai Serikali Sh8.43 trilioni. Mfuko wa PSPF unadai (Sh429 bilioni), PPF (Sh192 bilioni), NSSF (Sh467 bilioni), NHIF (Sh107 bilioni), LAPF (Sh170 bilioni) na GEPF (Sh6.8 bilioni).

Jumla hiyo ya deni la Serikali linahusisha deni jingine la PSPF la Sh7.06 trilioni ambayo ni malimbikizo ya madeni ya muda mrefu.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema kuwa mifuko hiyo huikopesha Serikali kupitia wizara mbalimbali, fedha ambazo hutakiwa kulipwa baada ya muda fulani.

Alisema wizara zisipolipa na hivyo deni kukaa kwa muda mrefu, huingizwa kwenye deni la Taifa.

“Madeni hayo ni makubwa, yanahitaji baraza la mawaziri kujadili utaratibu gani utatumika kulipa,” alisema Mwigulu na kuongeza:

“Kwa mfano deni la PSPF ni kubwa na linahitajika kulipwa, hivyo tunaweka utaratibu lakini siyo kwamba Serikali hailip... kama mwaka jana tuliilipa PSPF zaidi ya Sh50 bilioni sema nao wana mahitaji yao.”

Akizungumzia deni la MSD, Mwigulu alisema: “Hili la MSD tumetaka mchanganuo wa wizara na kila halmashauri jinsi gani fedha zilizotolewa kwa ajili ya dawa, zimetumika”.

Alisema mwaka jana Serikali ilitoa Sh47 bilioni kwaajili ya dawa katika wizara na halmashauri, lakini fedha zilizotumika kununulia dawa ni Sh7 bilioni tu.

“Nyingine wamefanyia mambo mengine na ndiyo maana tunasema hatuwezi tukawa tunatoa tu fedha bila kupewa mchanganuo wa fedha hizo zimefanyiwa
[3:18PM, 28/10/2014] Sanga: Mwigulu: Tutalipa deni la Sh8.4 Tril
Serikali imesema inaandaa utaratibu wa jinsi ia kulipa madeni inayodaiwa na taasisi za hifadhi ya jamii.
Dar es Salaam. Serikali imesema inaandaa utaratibu wa jinsi ia kulipa madeni inayodaiwa na taasisi za hifadhi ya jamii pamoja na Bohari ya Dawa (MSD).

Mifuko hiyo inaidai Serikali Sh8.43 trilioni. Mfuko wa PSPF unadai (Sh429 bilioni), PPF (Sh192 bilioni), NSSF (Sh467 bilioni), NHIF (Sh107 bilioni), LAPF (Sh170 bilioni) na GEPF (Sh6.8 bilioni).

Jumla hiyo ya deni la Serikali linahusisha deni jingine la PSPF la Sh7.06 trilioni ambayo ni malimbikizo ya madeni ya muda mrefu.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema kuwa mifuko hiyo huikopesha Serikali kupitia wizara mbalimbali, fedha ambazo hutakiwa kulipwa baada ya muda fulani.

Alisema wizara zisipolipa na hivyo deni kukaa kwa muda mrefu, huingizwa kwenye deni la Taifa.

“Madeni hayo ni makubwa, yanahitaji baraza la mawaziri kujadili utaratibu gani utatumika kulipa,” alisema Mwigulu na kuongeza:

“Kwa mfano deni la PSPF ni kubwa na linahitajika kulipwa, hivyo tunaweka utaratibu lakini siyo kwamba Serikali hailip... kama mwaka jana tuliilipa PSPF zaidi ya Sh50 bilioni sema nao wana mahitaji yao.”

Akizungumzia deni la MSD, Mwigulu alisema: “Hili la MSD tumetaka mchanganuo wa wizara na kila halmashauri jinsi gani fedha zilizotolewa kwa ajili ya dawa, zimetumika”.

Alisema mwaka jana Serikali ilitoa Sh47 bilioni kwaajili ya dawa katika wizara na halmashauri, lakini fedha zilizotumika kununulia dawa ni Sh7 bilioni tu.

“Nyingine wamefanyia mambo mengine na ndiyo maana tunasema hatuwezi tukawa tunatoa tu fedha bila kupewa mchanganuo wa fedha hizo zimefanyiwa nini,” alisema Mwigulu.

1 comment:

  1. asante sana especially kwa ahadi ya kulipa deni la bohari ya dawa, kipaumbele cha serikali kiwe ni AFYA, taasisi kama Muhimbili,OceanRoad na MIREMBE na kitengo cha mifupa MOI, ni sehemu nyeti na kimbilio la sisi wanyonge, tafadhali sana Naibu waziri, muweke sekta ya afya kwenye kipaumbele maana baba wa Taifa alisema adui wa Tanzania ni Maradhi, Ujinga na Umaskini, juhudi zifanyike, kwanini viongozi msifanye ziara za kushtukiza kwenye mahospitali mjioneee wananchi wanavyoteseka ?? haingii akili pesa za dawa zikicheleweshwa lakini viongozi wanatibiwa India na kwingineko kwa hela hiyo hiyo ya walipa kodi, tuna tumaini na serikali yetu na eneo mtakalozoa sifa ni Afya , tunaomba sana mlipe deni la AFYA, baba yangu mzazi amefariki kwa kensa , ni uchungu sana jamani

    ReplyDelete