Meneja wa shirika la SEMA, Ivo
Manyanku, akizungumza kwenye uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani,
siku ya choo duniani na wiki ya usafi wa mazingira nchini uliofanyika
katika kijiji cha Tulya wilaya ya Iramba. Kulia mwenye miwani ni mkuu wa
wilaya ya Iramba,Yahaya Nawanda.
Na Nathaniel Limu, Iramba
SHIRIKA lisilo la kiserikali la
Sustainable Environment Management Action (SEMA),linatarajia kutumia
zaidi ya shilingi 396 milioni kugharamia utekelezaji wa mradi wa usafi
mashuleni na mazingira kwa ujumla,katika shule saba ba kata saba za
wilaya ya Iramba.
Fedha hizo ni ufadhili kutoka shirika la WaterAid Tanzania.
Hayo yamesemwa na meneja wa SEMA,Ivo
Manyanku, wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa siku ya kunawa mikono
duniani,siku ya choo duniani na wiki ya usafi wa mazingirav nchini,
iliyofanyika katika kijiji cha Tulya wilayani Iramba.
Alitaja baadhi ya malengo ya mradi
huo, kuwa ni pamoja na kuhamasisha na kuelimisha wanafunzi na jamii kwa
jumla namna bora ya kunawa mikono.
Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa
Singida,Yahaya Nawanda, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa siku ya
kunawa mikono duniani, siku ya choo dunia na wiki ya usafi wa mazingira
nchini uliofanyika kimkoa katika kijiji cha Tulya wilayani humo.
“Pia kuwaelimisha wanafunzi wa kike
waliopevuka (kuvunja ungo) njia bora zitakazowasaidia kuwa wasafi
kipindi chote cha siku zao za hedhi”,alifafanua Ivo na kuongeza kwa
kusema;
“Shughuli zingine ni ujenzi wa vyoo
bora na kuwahamasisha wanafunzi na jamii kwa ujumla kuvitumia
kikamilifu.Tutawaelimisha na kuwaahamasisha kunawa mikono pindi
wanapotoka chooni kujisaidia”.
Kwa upnde wake afisa afya wa wilaya
ya Iramba,Yohana Dondi,alisema kuwa wilaya ya Iramba ina kaya zenye vyoo
bora ni aslimia 42,vyoo kubalika 52,vyoo visivyokubalika asilimia 18 na
bila vyoo,ni aslimia sita.
Kwa mujibu wa afisa huyo,nchi
zinazoendelea,asilimia 70-80 ya maradhi yote,yanasababishwa na
maambukizi yatokanayo na vinyesi,hivyo kuwa ni kisababishi namba moja
cha vifo.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu,ni Choo bora na mikono safi kwa afya bora,heshima na usawa”.
Spider man kutoka Temeke jijini
Dar-es-salaam akitoa burudani ya kutembea juu ya waya kwenye hafla ya
uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani, siku ya choo duniani na wiki
ya usafi wa mazingira nchini iliyofanyika katika kijiji cha Tulya wilaya
ya Iramba.
Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa
Singida,Yahaya Nawanda (wa nne kutoka kushoto) akitoa maelekezo juu ya
ujenzi wa choo bora cha shule ya msingi Tulya.Wa tatu kushoto ni meneja
wa shirika la SEMA,Ivo Manyanku.
Baadhi ya wakazi wa kata ya
Tulya,waliohudhuria uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani,siku ya
choo duniani na wiki ya usafi wa mazingira nchini uliofanyika katika
kijiji cha Tulya wilaya ya Iramba.(Picha zote na Nathaniel Limu).
No comments:
Post a Comment